Main Title

source : Parstoday
Jumatano

27 Machi 2024

13:43:37
1447199

Kiongozi Muadhamu: Muqawama usio na kifani wa vikosi vya Muqawama na watu wa Ghaza umeutukuza Uislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, Muqawama usio na kifani wa vikosi vya Muqawama na watu wa Ghaza umeutukuza Uislamu.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo katika mkutano na Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS pamoja na ujumbe aliofuatana nao.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ijumaanne jioni, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameuenzi muqawama na kusimama imara kusio na mfano kwa vikosi vya Muqawama wa Palestina na watu wa Ghaza na kusisitiza kuwa, subira ya kihistoria iliyoonyeshwa na watu wa Ghaza mbele ya jinai, unyama na ukatili wa utawala wa Kizayuni unaofanywa kwa uungaji mkono kamili wa Magharibi ni jambo adhimu mno ambalo kwa hakika limeutukuza Uislamu; na kinyume na matakwa ya adui, limeligeuza suala la Palestina kuwa suala kuu la ulimwengu.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, mauaji ya watu wa Ghaza na mauaji ya kimbari yanayofanywa katika eneo hilo yanamuathiri kila mwenye hisia za utu na akaongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita hata chembe kuunga mkono kadhia ya Palestina na wananchi wake wa Ghaza wanaodhulumiwa na waliosimama imara.

342/