Main Title

source : Parstoday
Jumatano

27 Machi 2024

13:45:12
1447202

Kutolewa pendekezo la kuanzisha klabu ya nyuklia ya BRICS kwa kuishirikisha Iran

Mkutano wa 13 wa kimataifa wa Atomexpo 2024 huko Sirius, Russia umetoa pendekezo la kuasisi klabu ya nyuklia ya nchi wanachama wa kundi la BRICS kwa kuishirikisha Iran.

BRICS ni jina la kundi linaloongozwa na mataifa yenye nguvu za kiuchumi, ambalo liliundwa kwa kuunganisha herufi za kwanza za majina ya Kiingereza ya Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. 

Uanachama rasmi wa Iran ndani ya kundi la BRICS ulikubaliwa katika mkutano wa 15 wa viongozi wa kundi hilo huko Johannesburg Afrika Kusini.  

Kirill Kamarov, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kwanza Anyehusika na Maendeleo ya Biashara na Biashara ya Kimataifa wa Kampuni ya ROSATOM. ya Russia ameashiria  katika mkutano wa 13 wa kimataifa wa Atomexpo 2024 uwezo wa kundi la BRICS katika uga wa nishati ya nyuklia na kupendekeza kuandaliwa utaratibu mpya wa ushirikiano katika kalibu ya nchi wanachama wa BRICS katika uwanja huo.   

Kamarov ameeleza kuwa nchi wanachama wa BRICS zinamiliki karibu asilimia 30 ya mitambo ya nyuklia inayofanya kazi duniani na karibu asilimia 70 ya viwanda vya nyuklia vinavyoendelea kujengwa.  

Wakati huo huo Hussein Derakhshandeh Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amekaribisha pendekezo la Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kwanza Anayehusika na Maendeleo ya Biashara na Biashara ya Kimataifa wa Kampuni ya ROSATOM ya Russia na kusema: Klabu ya nyuklia ya nchi wanachama wa BRICS inaweza kuwa na mchango athirifu katika kupunguza uzalishaji wa hewa ya kaboni na kuboresha maisha ya wananchi kupitia kustawisha tiba ya nyuklia na utoaji elimu kuiga mifano ya wazi ya miradi inayoitekekeleza. 

342/