Kwa mujibu wa ABC News, wizara ya fedha ya Marekani imetangaza kwamba Ofisi ya Udhibiti wa Mali za Kigeni (OFAC) imewawekea vikwazo watu wawili na asasi tatu kwa hoja kwamba ndio warahisishaji wakuu wa njia za kuipatia fedha Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS. Kwa mujibu wa tangazo la wizara ya fedha ya Marekani, GAZA NOW (Ghaza Sasa) na mwanzilishi wake Mustafa Ayash, pamoja na makampuni ya Al-Qureyshi Executive na Auzma Sultanah pamoja na mkurugenzi wa makampuni hayo mawili, wameshughulikia ukusanyaji wa misaada ya kifedha kwa ajili ya Hamas.Tovuti ya Kiarabu ya Gaza NOW ina zaidi ya wafuasi 300,000 kwenye mtandao wa kijamii wa X na idadi kubwa ya wafuasi kwenye jukwaa la maongezi la Telegram.
342/