Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

29 Machi 2024

13:57:39
1447633

Iran: Walimwengu wana wajibu wa kuubebesha dhima utawala wa Kizayuni

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameitaka jamii ya kimataifa ichukue hatua na kuubebesha dhima utawala wa Kizayuni, baada ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Palestina kufanya tathmini ambayo imezitaja jinai za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza kuwa ni mauaji ya kimbari.

Nasser Kan'ani amesema katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa X jana Alkhamisi kuwa: Jinai ya mauaji ya kimbari inayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina sasa imethibitishwa na Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa.

Kan'ani amesema: Serikali za kitaifa na mashirika ya kimataifa ya kisiasa na kisheria sasa yanawajihiwa na hukumu si tu ya mtazamo wa umma, bali pia ya kihistoria. Je yatatekeleza majukumu yao ya kibinadamu, kisheria na kihistoria?

Siku ya Jumanne,  Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Anayehusika na Masuala ya Haki za Binadamu ya Palestina aliwasilisha ripoti yake kuhusu Gaza kwa Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo huko Geneva, Uswisi ambapo alifikia natija kwamba utawala wa Kizayuni unatekeleza mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.Albanese amezitaka nchi za dunia kuuwekea utawala wa Kizayuni vikwazo vya silaha na vikwazo vinginevyo. Hata hivyo utawala wa Kizayuni umekadhibisha yale yaliyoelezwa ndani ya ripoti ya Francesca Albanese huku mashinikizo ya kimataifa yakiongozeka kwa utawala huo ili usimamishe vita vyake vya mauaji ya kimbari huko Gaza haraka iwezekanavyo. Wakati huo huo makumi ya wanadiplomasia, wengi wao wakiwa ni wanadiplomasia wa ngazi za juu wa nchi za Kiarabu na Kiislamu na pia kutoka Amerika ya Latini wameunga mkono na kupongeza ripoti hiyo ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Anayehusika na Masuala ya Haki za Binadamu ya Palestina katika Baraza la Haki za Binadamu la UN. 

342/