Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Machi 2024

17:37:46
1448029

Wapalestina zaidi ya 400 wameuawa shahidi katika hospitali ya al Shifa iliyozingirwa

Vyombo vya habari kutoka Ukanda wa Gaza vimetangaza kuwa Wapalestina zaidi ya 400 wameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel katika Hospitali ya al Shifa ambayo inaendelea kuzingirwa na utawala wa Kizayuni kwa siku ya 13 sasa.

Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Gaza imetangaza katika taarifa yake kwamba wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanatekeleza uhalifu wa aina mbalimbali wakati wa mashambulizi na hujuma za kikatili katika hospitali hiyo ya Gaza ambayo ni kituo kikubwa zaidi cha matibabu katika eneo hilo linalohifadhi maelfu ya wagonjwa na watu waliokimbia makazi yao. Wanajeshi wa Israel wameshambulia, kubomoa na kuchoma nyumba 1,050. 

Taarifa ya idara hiyo imeongeza kuwa wahanga wa hujuma za Israel katika Hospitali ya al Shifa ni pamoja na wagonjwa, raia wa Kipalestina waliokimbia vita na wafanyakazi wa tiba na kwamba mamia ya wengine wametiwa nguvuni na kukabiliwa na mateso. 

Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Gaza imekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa kwa jinai za Israel katika eneo la Hospitali ya al Shifa na kuibebesha dhima serikali ya Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi kwa kushirikiana na utawala wa Israel katika umwagaji damu ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. 

Dakta Hossam Abu Safiya Mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan huko Jabalia, kaskazini mwa Gaza, ameeleza kuwa wafanyakazi wa hospitali hiyo wanafanya kazi katika mazingira magumu.  Machi 18 mwaka huu wanajeshi wa utawala wa kizayuni waliokuwa wamejizatiti kwa silaha mbalimbali waliishambulia Hospitali ya al Shifa kwa vifaru na ndege zisizo na rubani huku wakiwafyatulia risasi watu ndani ya hospitali hiyo. 

342/