Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Machi 2024

17:38:50
1448031

Licha ya kuikosoa Israel hadharani, Biden ameidhinisha kwa siri silaha mpya za kuwaulia Wapalestina

Rais Joe Biden wa Marekani hivi karibuni ameidhinisha kwa siri kupatiwa utawala wa Kizayuni wa Israel silaha mpya za kivita zenye gharama ya mabilioni ya dola zikiwemo aina za kisasa za mabomu na ndege za kivita.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyofichuliwa na gazeti la Washington Post licha ya maafisa wa Marekani kueleza hadharani wasiwasi wao juu ya kuongezeka vifo vya Wapalestina katika vita vya kikatili vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya eneo la Ghaza uliloliwekea mzingiro.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Washington imezipata kwa maafisa wa wizara ya mambo ya nje na ya ulinzi Pentagon ambao hawakutaka kutajwa majina yao, silaha zilizoidhinishwa wiki hii na rais wa Marekani kwa ajili ya Israel ni pamoja na mabomu hatari 1,800 ya MK84 yenye uzito wa pauni 2,000 na mabomu 500 aina ya MK82 yenye uzito wa pauni 500.Afisa mmoja wa serikali ya Washington amesema, wiki iliyopita wizara ya mambo ya nje iliidhinisha utumaji wa ndege na injini 25 za kivita aina ya F-35A. Ndege na injini hizo zinakadiriwa kuwa na thamani ya karibu dola bilioni 2.5. Mauzo hayo hayajawekwa hadharani, na hakuna matangazo yanayohusiana na suala hilo yaliyowekwa kwenye tovuti ya Wakala wa Ushirikiano wa Usalama wa Ulinzi ambako kwa kawaida hutumwa taarifa kama hizo. Siku ya Ijumaa, Seneta Bernie Sanders alikosoa hatua ya serikali ya Biden ya kuidhinisha utumaji silaha zaidi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa X, Sanders amlishiria ripoti ya Washington Post na kusema: "Marekani haiwezi siku moja kumsihi Netanyahu aache kuwashambulia raia kwa mabomu, kisha siku inayofuata kumpelekea maelfu ya mabomu ya pauni 2,000 ambayo yanaweza kusagasaga majengo ya jiji zima. Huuu ni uchafu". Unafiki huo wa Biden umefichuliwa wakati rais huyo wa Marekani na waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu wameonyesha kuzozana hadharani katika wiki za hivi karibuni juu ya raia Wapalestina wanaouawa kwa wingi huko Ghaza, karibuni zaidi ikiwa ni baada ya Marekani kutopigia kura ya turufu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka kusitishwa mara moja mapigano katika eneo hilo.../

342/