Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Machi 2024

17:39:22
1448032

61% ya Waisraeli hawaamini kama vita vya Ghaza vitamalizika kwa kusambaratishwa HAMAS

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa Palestina inayokaliwa kwa mabavu iliyopandikizwa jina bandia la Israel yanaonyesha kuwa asilimia 61 ya Wazayuni hawaamini kama vita vya Ghaza vitamalizika kwa "kusambaratishwa harakati ya Hamas".

Matumaini ya kufikiwa mwafaka kati ya Hamas na utawala wa Kizayuni yanazidi kufifia kuliko ilivyokuwa hapo awali, huku mpasuko ukishuhudiwa ndani ya baraza la mawaziri la waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu sambamba na maoni ya umma katika utawala huo yakionyesha kuwepo wasi wasi wa vita kusababisha mtikisiko mkubwa bila ya Tel Aviv kufikia malengo ya kuiangamiza Hamas na kuwakomboa mateka wa Kizayuni. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Wanachuo wa Iran (ISNA), matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na kanali ya 13 ya televisheni ya Israel siku ya Ijumaa yameonyesha kuwa, asilimia 59 ya Wazayuni wanaamini pia kwamba, hali ya usalama kwenye makazi yao huko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu ambako kuna mapigano yanayoendelea mtawala kati ya jeshi la Israel na Hizbullah ya Lebanon, itakuwa mbaya zaidi.Viongozi wa utawala wa Kizayuni wanadai kuwa watasimamisha vita katika Ukanda wa Ghaza baada tu ya kufikiwa malengo ya vita hivyo yakiwemo ya kuangamizwa Hamas na kukombolewa mateka; malengo ambayo hadi sasa bado hayajaweza kufikiwa kivitendo. Meja Jenerali Itzhak Brik, kamanda wa kikosi cha akiba cha jeshi la Israel amesema, ikiwa vita vitaendelea, si baidi vikapelekea kuangamia Israel. Brik ameongeza kuwa, "kuiangamiza kikamilifu Hamas," kama anavyokariri kila siku Netanyahu, ni kauli mbiu tupu isiyo na msingi wowote.../

342/