Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Machi 2024

17:39:53
1448033

Kwa mnasaba wa "Siku ya Ardhi", HAMAS yautolea wito Umma wa Kiislamu kuikomboa Palestina

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa taarifa maalumu kwa mnasaba wa "Siku ya Ardhi" ikisisitiza kuwa kuikomboa ardhi ya Palestina na matakatifu yake ni jukumu la Umma wote wa Kiislamu.

Tarehe 30 Machi 1976 viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walipora maelfu ya hekta za ardhi ya Wapalestina katika eneo la Al-Jalil lililoko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kufuatia kitendo hicho cha jinai, Wapalestina walianzisha mgomo wa kususia kula na maandamano ya upinzani.Maandamano hayo ya Wapalestina yalisababisha makabiliano makali kati yao na jeshi la Israel, ambapo Wapalestina sita waliuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa Kizayuni na maelfu ya wengine walijeruhiwa.Kwa sababu hiyo, wananchi wa Palestina wanaiadhimisha tarehe 30 Machi kila mwaka kwa lengo la kuwakumbuka na kuwaenzi Mashahidi wa mwaka 1976 na kufanya maandamano katika siku hiyo ya kupinga Uzayuni. Siku hii inaitwa "Siku ya Ardhi".Kwa mujibu wa televisheni ya Al-Quds, harakati ya Hamas imesisitiza kuwa, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni muendelezo wa mapinduzi ya wananchi wa Palestina katika kulinda ardhi na maeneo yao matakatifu.

Taarifa ya Hamas imeeleza kwamba, ardhi ya kihistoria ya Palestina, ambayo kitovu chake ni Al-Quds na Msikiti wa Al-Aqsa ndio mhimili mkuu wa mapambano na adui, na hakuna njia nyingine ya kuikomboa isipokuwa Muqawama wa kila upande.

Taarifa ya harakati hiyo ya Muqawama imesema, "HAMAS inauenzi ushujaa na kujitolea mhanga kwa Muqawama na hamasa ya wananchi wetu katika Ukanda wa Ghaza na inawataka watu wake katika Ukingo wa Magharibi, Al-Quds, Msikiti wa Al-Aqsa na katika kambi za wakimbizi kuwa na mshikamano zaidi na kuimarisha aina zote za Muqawama.

Taarifa ya Hamas imesisitiza kuwa, kukombolewa ardhi ya Palestina, Al-Quds, Msikiti wa Al-Aqsa na maeneo matakatifu, kuhitimishwa ukaliaji ardhi kwa mabavu na kuundwa taifa huru la Palestina ambalo mji mkuu wake ni Baitul Muqaddas, hakulihusu taifa la Palestina pekee, bali ni jukumu la kihistoria lililoko juu ya mabega ya Umma wa Kiarabu na Kiislamu pamoja na watu wenye fikra huru duniani kote; na harakati hiyo, inautaka Umma wa Kiarabu na Kiislamu na watu huru duniani kuzidisha mshikamano na uungaji mkono wao kwa watu wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza.../

342/