Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Machi 2024

17:40:34
1448034

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA: Iran haina silaha za nyuklia

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) ametenganisha baina ya kategoria ya kurutubisha madini ya urani na mchakato wa uundaji silaha za nyuklia na kutangaza kuwa Iran haitengenezi silaha za nyuklia licha ya kuwa na akiba ya urani iliyorutubishwa.

Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya PBS ya Marekani, Rafael Grossi  amesema: "Iran ina akiba kubwa ya urani iliyorutubishwa kwa kiwango cha juu; na jambo hili limetoa msukumo kwa wakala wa IAEA kuwa makini kwa sababu hakuna nchi ambayo haina silaha za nyuklia ambayo hairutubishi kwa kiwango hiki." 

Grossi ameeleza kuwa uundaji wa silaha za nyuklia ni mchakato mgumu unaohitaji hatua zaidi. 

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA)  ameashiria pia hatua za fidia za Iran katika mapatano ya JCPOA na kukariri madai kuhusu kupungua ufikaji wa wakaguzi katika maeneo ya Iran na kusema: Kama itatokea siku mapatano ya JCPOA yakaanza kutekelezwa kwa mara nyingine, basi utendaji wa wakala wa IAEA utakuwa mgumu kutokana na kuendelea hali ya sasa.Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia imesisitiza mara kadhaa kuwa hatua za fidia zilizotekelezwa katika mapatano ya JCPOA haziathiri moja kwa moja au kinyume chake uwezo wa wakala huo katika kutekeleza shughuli zake za ukaguzi nchini Iran. 

342/