Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Machi 2024

17:43:53
1448040

Watu masikini na wakimbizi wafukuzwa Paris kabla ya Olimpiki

Takriban wakimbizi 500 na watu masikini wasio na makazi wamehamishwa kwa nguvu kutoka mji mkuu wa Ufaransa na kupelekwa maaeneo ya vijijini na miji midogo nchini humo huku Paris ikijiitayarisha kuandaa Olimpiki ya Majira ya joto ya 2024 mnamo Julai na Agosti.

Hatua hiyo imetajwa na wanaharakati wa kibinadamu na baadhi ya mamlaka za mitaa kama jaribio la kuwaficha wasio na makazi kabla ya tukio hilo na hivyo kuwasilisha taswira bandia ya Paris kwa wageni.

Baadhi ya mameya wa mikoa wameelezea wasiwasi wao juu ya wahamiaji hao wapya katika mikoa yao. Serge Grouard, meya wa Orleans katikati mwa Ufaransa, eneo lenye wakazi karibu 100,000, amewaambia waandishi wa habari kwamba kumekuwa na uvumi kwamba hatua hiyo inalenga "kusafisha taswira" katika mji mkuu kabla ya Olimpiki.

Paul Alauzy wa NGO ya Medecins du Monde ameiambia Euronews kwamba serikali imezindua kampeni ya kuufanya mji mkuu wa Ufaransa uwe msafi zaidi lakini kama wazo ni kuficha huzuni na ukosefu wa makazi kabla ya Olimpiki na kuwa jambo hilo halifanyiki katika kiwango cha kibinadamu.

Ufaransa ilipokea maombi 167,000 ya hifadhi mwaka 2023, idadi kubwa ya pili katika Umoja wa Ulaya, ikiwa na wahamiaji wengi kutoka Afrika, Asia Kusini, na Mashariki ya Kati.

Mahitaji ya malazi ya muda mfupi ya dharura ni zaidi ya uwezo ambapo kambi za muda huibuka mara kwa mara karibu na mji mkuu na hatimaye kuvamiwa na kuvunjwa na polisi.

342/