Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Machi 2024

17:45:40
1448041

Zelensky aonya: Bila msaada wa kijeshi wa Marekani, Ukraine italazimika kurudi nyuma

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema iwapo nchi yake haitopatiwa msaada wa kijeshi ulioahidiwa na Marekani ambao kwa sasa umezuiwa kutokana na mizozo iliyomo ndani ya Kongresi ya nchi hiyo italazimika kurudi nyuma katika vita na Russia hatua kwa hatua.

Katika mahojiano na gazeti la The Washington Post, Zelensky amefikisha ujumbe wa kijasiri kwa bunge la Kongresi la Marekani, akilitaka liipatie silaha nchi yake ili kukomesha mashambulizi ya Russia, vinginevyo Ukraine itazidisha mashambulizi yake dhidi ya viwanja vya ndege vya Russia, vituo vya nishati na maeneo mengine ya kimkakati. Katika mahojiano hayo, rais wa Ukraine amebainisha kuwa, kuchelewesha bunge la Marekani kuidhinisha fungu la msaada wa kijeshi la dola bilioni 60 kumeitia gharama kubwa nchi yake. Amesema: "ikiwa hakuna usaidizi wa Marekani, maana yake ni kwamba hatuna ulinzi wa anga, hakuna makombora ya Patriot, hakuna mitambo kwa ajili ya vita vya elektroniki na hakuna risasi za milimita 155. Inamaanisha tutarudi nyuma, ni kurudi nyuma hatua kwa hatua, katika hatua ndogondogo."Alipoulizwa kama Ukraine inakosa vipokezi na silaha nyingine za ulinzi wa anga kwa ajili ya kulinda miji na miundombinu yake, Zelensky alijibu kwa kukiri na kuthibitisha akisema: "hiyo ni kweli. Sitaki Russia ijue ni idadi gani ya makombora ya ulinzi wa anga tunayo, lakini kimsingi, uko sawa. Bila kuungwa mkono na Kongresi, tutakuwa na upungufu mkubwa wa makombora. Hili ndilo tatizo. Tunaongeza mifumo yetu ya ulinzi wa anga, lakini haitoshi".

Rais Joe Biden ametoa wito kwa Baraza la Wawakilishi la Marekani linaloongozwa na chama cha Republican kuunga mkono msaada wa kijeshi na kifedha; hata hivyo, Spika wa Bunge Mike Johnson amechelewesha suala hilo kwa miezi kadhaa, akielezea sababu za wasiwasi wa ndani.

Wakati wa mazungumzo yao ya simu siku ya Alhamisi, Zelensky alimsisitizia Johnson umuhimu wa kuidhinisha fungu hilo la msaada wa kijeshi.

Naye Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amelihimiza bunge la Kongresi liidhinishe nyongeza ya bajeti ya Usalama wa Taifa iliyoombwa na Biden ili kuisaidia Ukraine dhidi ya Russia.../


342/