Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

1 Aprili 2024

14:12:29
1448207

Kwa mara nyingine, Hizbullah yazitwanga kwa mizinga kambi za kijeshi za Israel

Wanamapambano wa Kiislamu wa nchini Lebanon kwa mara nyingine wamezitwanga kwa mizinga kambi za kijeshi za utawala wa Kizayuni wa Israel kujibu jinai na mauaji ya umati yanayofanywa na Wazayuni huko Ghaza, Palestina.

Hizbullah ya Lebanon imefanya mashambulizi kadhaa ya mizinga dhdi ya kambi za utawala wa Kizayuni kama sehemu ya kupigana bega kwa bega na wanamuqawama wa Palestina kwenye Ukanda wa Ghaza ambao wanakabiliana kiume na jinai za utawala pandikizi wa Israel.

Mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi ya Hizbullah ya Lebanon yamewatia hofu kubwa wanajeshi woga wa Israel katika vitongoji vya Wazayuni vya kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel. 

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kunukuu taarifa ya Hizbullah ya Lebanon ikisema kuwa, harakati hiyo ya Kiislamu imezipiga kwa mizinga kambi mbili za kijeshi za Israel kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na imetumia makombora ya Burkan kuzipiga kambi hizo.

Mashambulizi hayo ya Hizbullah yamekuja kujibu pia mashambulio ya ndege za utawala wa Kizayuni katika baadhi ya maeneo ya kusini mwa Lebanon. 

Hizbullah imeingia vitani kupambana na utawala wa Kizayuni tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya maangamizi ya kizazi kwenye Ukanda wa Ghaza huko Palestina tarehe 7 Oktoba 2023.

342/