Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

1 Aprili 2024

14:21:40
1448216

UNICEF yaonya kuhusu hali ya kutisha ya vita kwa watoto wa Ghaza

Msemaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto ameonya kuhusu hali mbaya na ya kutisha waliyo nayo watoto wa ukanda wa Ghaza ambao wanateseka kwa mambo mengi ikiwemo njaa na mashambulizi ya mfululizo ya wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni.

Msemaji wa UNICEF, James Elder, amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba watoto wa Ukanda wa Ghaza wanaishi katika hali na mazingira ya kutisha yanayotokana na mashambulizi ya mfululizo ya Israel pamoja na njaa iliyosababishwa na kuzingirwa kikamilifu Ukanda wa Ghaza. 

Ameelezea kusikitishwa sana na jinsi dunia inavyoangalia kwa macho tu watoto wa Ghaza wanavyoteseka na kusema kuwa, watoto wa ukanda huo wanapoteza maisha kila siku mbele ya macho ya walimwengu ambao hawachukui hatua yoyote ya maana ya kuokoa maisha ya maelfu ya watoto wa eneo hilo. 

Licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitaka Israel ikomeshe mara moja jinai zake huko Ghaza na licha ya dunia nzima kulaani ukatili wa kupindukia unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel, lakini Israel inaendelea kufanya kiburi na kupuuza malalamiko yote hayo na hadi hivi sasa umeshaua shahidi karibu Wapalesetina 33,000 na kujeruhi wengine zaidi ya 75,000 tangu ulipoanzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya eneo na ukanda huo mdogo wa Ghaza, tarehe 7 Oktoba 2023.

342/