Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

1 Aprili 2024

14:22:16
1448217

Wataalamu na wanasiasa: Israel haidhibitiki, asiyeiadhibu ni mshirika katika uhalifu

Wataalamu na wanasiasa wanasema Israel imefikia hatua ya unazi ambayo haiwezi kuvumiliwa na kwamba Marekani, nchi za Magharibi na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ni washirika katika jinai zinazofanywa na utawala huo zikiwemo nchi za Kiarabu ambazo hazikuchukua hatua yoyote kuiadhibu Israel baada ya uamuzi wa hivi karibuni wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa ulazima wa kusitisha mapigano mara moja huko Gaza.

Matamshi ya wachambuzi hao yamekuja baada ya jeshi la Israel kukiri kuwa liliwaua vijana wawili wa Kipalestina walipokuwa wakirejea kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kupitia Mtaa wa Al-Rashid, wakiwa wamebeba bendera nyeupe. 

Jeshi la Israel limehalalisha mauaji hayo kwa kudai kwamba, mauaji ya Wapalestina hao wawili yalitokea baada ya kukaribia eneo la operesheni katikati mwa Gaza kwa njia ya kutia shaka.

Hata hivyo, picha za video zilizonaswa na televisheni ya Al Jazeera ya Qatar zinaonyesha wanaume wawili wa Kipalestina wasio na silaha, mmoja akipunga hewani kitambaa cheupe mara kwa mara kuashiria kujisalimisha, kabla ya askari katili wa jeshi la kigaidi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuwapiga risasi na kisha kuzifukia maiti zao kwenye kifusi kwa kutumia tingatinga karibu na mji wa Gaza.

Akizungumzia kukiri kwa Israel kuwaua vijana hao wawili wa Kipalestina kulikofichuliwa na televisheni ya Al Jazeera, mbunge wa Bunge la Ireland, Richard Boyd Barrett, amesema kuwa suala hilo haliwezi kukanushwa kwa sababu likesajiliwa.

Boyd Barrett amesema: "Matendo haya na mengine "yanathibitisha kwamba tunakabiliwa na utawala ambao haujali sheria za kibinadamu na haujali yanayosemwa na walimwengu."

Barrett anaamini kwamba Israel "imetoka kwenye udhibiti kabisa" na kwamba swali muhimu zaidi sasa ni "Je, wafadhili wa Kimagharibi ambao wanaendelea kuipatia silaha, licha ya mauaji haya ya kimbari, watachukua hatua kukomesha vitendo hivi?"

Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kimataifa Dk. Saad Jabbar anasisitiza kwamba, kinachofanywa na jeshi la Israel katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza "kinathibitisha kuwepo kwa nia ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina."Amesisitiza kuwa, Akisisitiza kwamba mhusika mkuu wa mauaji haya ya kimbari ni Rais wa Marekani Joe Biden, "ambaye anaishi mbali mbali kabisa na ustaarabu wa binadamu." Kwa upande wake, Dk. Mustafa Barghouthi amemtuhumu Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Karim Khan, kuwa anashirikiana na Israel kwa sababu ya "kuwa bubu" na kunyamazia kimya uhalifu unaofanywa na utawala huo huko Palestina. Barghouti amesisitiza ulazima wa kuiwekea Israel vikwazo ili kutekeleza maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, “kama ilivyotokea kwa Russia, ambayo iliwekewa vikwazo 11,000 kuhusiana na vita vya Ukraine ndani ya miezi miwili, wakati nchi za Magharibi hazijachukua hatua yoyote kwa ajili ya Wapalestina hadi leo". 

342/