Main Title

source : Parstoday
Jumanne

2 Aprili 2024

14:36:02
1448517

Kwa mara nyingine, Oman yalaani shambulio la Israel kwenye ubalozi wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amelaani shambulio la kigaidi lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjiini Damascus Syria. Kabla ya hapo Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman iliikuwa imetoa taarifa rasmi ya kulaani shambuliizi hilo la kigaidi.

Sayyid Badr bin Hamad Al-Busaidi amesema hayo kwenye mazungumzo ya simu aliyofanya na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Iran, Hussein Amir-Abdollahian na kusisitiza kuwa, shambulio lolote dhidi ya maeneo ya kidiplomasia halikubaliki na halihalalishiki kwa namna yoyote ile. Amesema shambulio hilo limekanyaga maazimio na mikataba yote ya Umoja wa Mataifa na ya kimataifa.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wametilia mkazo pia wajibu wa kufanyika juhudi za kimataifa za kukomesha haraka jinai za utawala wa Kizayuni kwenye Ukanda wa Ghaza.

Mbali na Oman, nchi nyingine duniani kama Russia, Pakistan, Saudi Arabia, Imarati na Qatar nazo zimeungana na mataifa mengine kuulaani utawala haramu wa Israel kwa shambulizi lake la kigaidi katika ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus, Syria.

Shambulizi hilo la makombora lililofanywa jana na utawala wa Kizayuni kutokea eneo la Golan unalolikalia kwa mabavu dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, limepelekea kuuawa shahidi maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi wa Iran kama Jenerali Mohammad Reza Zahedi na Jenerali Mohammad Hadi Haj Rahimi pamoja na watu wengine watano waliokuwa pamoja nao.

Jana usiku, Faisal Miqdad, Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria alifika katika ubalozi wa Iran na kulaani shambulio la hilo na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni kamwe hautaweza kuvuruga uhusiano kati ya Syria na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

342/