Main Title

source : Parstoday
Jumanne

2 Aprili 2024

14:37:45
1448521

Askari wa Israel wakiri, wengi waliowaua Ghaza kama 'magaidi' ni raia wa kawaida

Maafisa na askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamekiri kuwa akthari ya vifo vilivyoelezewa na jeshi hilo kuwa ni vya kuua "magaidi" wakati wa vita vyake dhidi ya Ukanda wa Ghaza, kiukweli hasa ni vya mauaji ya raia wa kawaida.

Gazeti la Israel la Haaretz limekusanya na kuchapisha ushuhuda uliotolewa na maafisa na askari wa jeshi la Kizayuni ambao wamepigana huko Ghaza katika vita ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu Oktoba 7, 2023. Ripoti ya gazeti hilo imeeleza kwamba: "jeshi la Israel linasema, magaidi 9,000 wameuawa tangu vilipoanza vita vya Ghaza". Hata hivyo, maafisa na wanajeshi wa Israel wameliambia Haaretz kwamba "mara nyingi hawa huwa ni raia ambao uhalifu pekee waliofanya ulikuwa ni kuvuka mstari usioonekana, uliochorwa na jeshi la Israel". Askari mmoja ameliambia gazeti hilo: "tuliambiwa wazi kwamba hata ikiwa mshukiwa anaingia kwenye jengo lenye watu ndani yake, tunapaswa kufyatua risasi kwenye jengo hilo na kumuua gaidi, hata ikiwa watu wengine watajeruhiwa".Kwa mujibu wa ushuhuda wa maafisa na askari wa Kizayuni, jeshi la Israel hufyatua risasi kwa mtu yeyote anayeingia katika lililoainishwa kuwa "eneo la mauaji", awe mtu mwenye silaha au raia.

 Afisa mmoja wa akiba wa jeshi la utawala wa Kizayuni ameliambia Haaretz: “kimsingi, gaidi ni mtu yeyote ambaye jeshi limemuua katika maeneo ambayo askari wake wanaendesha shughuli zao.” Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu anakabiliwa na ukosoaji mkubwa wa raia wa utawala huo wa Kizayuni kwa kushindwa kufikia malengo ya vita dhidi ya Ghaza, hasa ya kuliangamiza kundi la Muqawama wa Palestina la Hamas na kuwakomboa mateka wa Israel.../

342/