Main Title

source : Parstoday
Jumanne

2 Aprili 2024

14:38:42
1448523

Kiongozi Muadhamu: Iran itaufanya utawala wa Israel ujutie uhalifu nchini Syria

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Majenerali walioongoka wa Kiislamu katika shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria na kusisitiza kwamba: "Taifa la Iran litawafanya Wazayuni wajutie jinai hiyo na jinai zingine kama hiyo."

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake leo Jumanne ameongeza kuwa: "Majenerali waliongoka na waliojitolea wa Kiislamu, Meja Jenerali Mohammed Reza Zahedi  na mpiganaji mwenzake  Mohammed Hadi Haj Rahimi wameuawa shahidi katika jinai ya utawala ghasibu na unaochukiwa wa Kizayuni."

Ayatullah Khamenei amesema: "Amani na rehema za Mwenyezi Mungu na mawalii wake ziwe juu yao na  mashahidi wengine wa tukio hili, na laana ziwashukie viongozi wa utawala dhalimu na vamizi wa Israel. Mashahidi walipokea ishara ya kukubaliwa mapambano yao ya muda mrefu kutoka kwa Mwenyezi Mwenye Rehema, na sasa wako pamoja na mawalii na watu wema kwa baraka na neema za Mwenyezi Mungu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Wapiganaji shujaa wa Kiislamu watuadhibu utawala khabithi wa Israel unaotekeleza mauaji ya kimbari na wataufanya ujutie jinai hiyo na jinai zingine kama hiyo."
Jana Jumatatu jino, ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zililenga ubalozi mdogo wa Iran  katika Mtaa wa Al-Mezeh huko Damascus.
Kutokana na uchokozi huo, watu saba wakiwemo wanadiplomasia na maafisa wa mwambata wa kijeshi katika ubalozi wa Iran waliuawa shahidi.

342/