Main Title

source : Parstoday
Jumanne

2 Aprili 2024

14:39:03
1448524

Rais Raisi: Wazayuni kamwe hawatofikia malengo yao haramu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia jinai na ugaidi uliofanywa jana Jumatatu na utawala wa Kizayuni wa kushambulia ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus Syria na kusema kuwa, Wazayuni wanapaswa kutambua kwamba ugaidi wao wa kinyama kama huo hauwezi kuwafanikishia malengo yao maovu.

Jana jioni (Aprili Mosi 2024), utawala wa Kizayuni ulishambulia ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus na kuua shahidi washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu akiwemo Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) nchini Syria na Lebanon, Brigedia Jenerali Mohammad Reza Zahedi na naibu wake, Mohammad Hadi Haji Rahimi na watu wengine watano.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Rais Ebrahim Raisi akilaani ugaidi na jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni ambayo imekanyaga sheria zote za kimataifa za wajibu wa kuheshimiwa maeneo ya kidiplomasia na kusisitiiza kuwa, maafisa hao wa Iran wamefanikiwa kupata daraja ya juu ya kuuawa shahidi katika njia ya Quds na kulinda Haram za Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad SAW.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, utawala ghasibu wa Kizayuni umefanya shambulio hilo la kipunguani na kiwendawazimu baada ya kuchezea vipigo mtawalia katika medani za mapambano baina yake na kambi ya muqawama.

Kwa mara nyingine amesisitiza kwa kusema: Wazayuni waelewe kwamba vitendo vyao hivyo vya kinyama kamwe havitawasaidia kufanikisha malengo yao haramu na maovu, bali siku baada ya siku tutaendelea kushuhudia jinsi kambi ya muqawama inavyozidi kuwa imara na hasira za mataifa ya dunia zinavyozidi kuongezeka dhidi ya utawala katili na pandikizi wa Israel.

342/