Main Title

source : Parstoday
Jumanne

2 Aprili 2024

14:39:25
1448525

Iran: Utawala wa Kizayuni ni tishio kwa usalama na amani ya dunia nzima

Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa na taasisi nyinginezo za kimataifa huko Geneva Uswisi amelaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus Syria na kusema kuwa Israel ni utawala unaohatarisha usalama wa dunia nzima na unapuuza kikamilifu hati ya Umoja wa Mataifa.

Shirika la habari la Tasnim limemnukuu mwakilishi huyo wa Iran katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao yao mjini Geneva Uswisi akisema hayo kwenye mtandao wa kijamii ya X na kuongeza kukwa, vitendo vya kijinai na vya uharibifu vya utawala wa Israel vimesababisha ukosefu na amani na utulivu kwenye eneo la Asia Magharibi.

Ndege za utawala wa Kizayuni jana Jumatatu jioni zilishambulia ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus Syria na kuua shahidi watu saba ambao ni maafisa wa kibalozi na washauri wa kijeshi wa Iran.

Hossein Akbari, balozi wa Iran mjini Damascus ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia kinyama sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria kinyume na mikataba yote ya kimataifa na kuwalenga waambata rasmi wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa Balozi Akbari, utawala wa Kizayuni umetumia ndege ya kivita ya F-35 kuushambulia kwa makombora 6 ubalozi huo mdogo wa Iran na kusisitiza kuwa, Israel imevuka mistari mekundu ya kimataifa na isubiri majibu makali ya Iran kwa jinai yake hiyo. 

342/