Hossein Akbari, balozi wa Iran mjini Damascus ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia kinyama sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria na kinyume na mikataba yote ya kimataifa na kuwalenga waambata rasmi wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.Kufuatia shambulio hilo la kigaidi lililofanywa na utawala wa Israel katika sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus na kupelekea kuuawa shahidi baadhi ya washauri rasmi wa kijeshi wa Iran, balozi mdogo wa Uswisi mjini Tehran ameitwa Wizara ya Mambo ya Nje akiwa msimamiaji wa maslahi ya Marekani nchini Iran, na kubainishiwa ukubwa wa shambulio la kigaidi na jinai hiyo iliyofanywa na utawala wa Israel ikisisitizwa kuwa serikali ya Marekani ndiyo inayobeba dhima hiyo.Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, salamu muhimu zimetumwa kwa serikali ya Marekani ikiwa ni muungaji mkono wa utawala wa Kizayuni, na Washington itapaswa kuwajibika.
342/