Main Title

source : Parstoday
Jumanne

2 Aprili 2024

14:42:01
1448531

Utawala wa Kizayuni washambulia jengo la ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria

Utawala ghasibu wa Kizayuni umetekeleza shambulio la anga dhidi ya jengo la ubalozi mdogo wa Iran karibu na ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Damascus Syria.

Vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimetangaza kuwa jana alasiri jeshi la utawala wa Kizayuni lilitekeleza shambulio la anga katika ubalozi mdogo wa Iran karibu na ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Damascus kutokea upande wa eneo la miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, shambulio la anga la utawala wa Kizayuni limeharibu kikamilifu jengo la ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus na kuwauwa shahidi na kuwajeruhi wafanyakazi kadhaa wa ubalozi huo mdogo.  

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) nchini Syria na Lebanon Brigadia Jenerali Mohammad Reza Zahedi na Naibu wake Mohammad Hadi Haji Rahimi ni kati ya watu waliouliwa shahidi katika shambulio la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus jana Jumatatu.

Kufuatia hujuma hiyo ya jeshi la utawala wa Kizayuni, Faisal Miqdad Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria jana usiku alifika katika ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kulaani shambulio la jeshi la utawala wa Kizayuni katika ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Damascus. Amesema utawala wa Kizayuni kamwe hautaweza kuvuruga uhusiano kati ya Syria na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 Wakati huo huo Hussein Akbari balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaeleza waandishi wa habari kuwa utawala wa Kizayuni umeushambulia ubalozi mdogo kwa makombora sita na kwamba yeye wakati huo alikuwa ofisini mwake ndani ya ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

342/