Main Title

source : Parstoday
Jumatano

3 Aprili 2024

20:47:03
1448814

Baraza la Usalama UN lalaani mashambulizi ya Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran, Damascus

Wawakilishi waliohudhuria kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus (mji mkuu wa Syria) wamelaani kitendo hicho cha kinyama cha Wazayuni.

Katika kikao hicho cha dharura kilichofanyika jana Jumanne, wawakilishi wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walilaani shambulio la hivi karibuni la Israel dhidi ya sehemu ya ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria, na kuonya juu ya matokeo mabaya ya uhalifu na kitendo hicho kinachokiuka sheria za kimataifa.Baada ya kushindwa utawala wa Kizayuni dhidi ya wanamapambano wa Palestina na Muqawama wa wananchi wa Gaza, Jumatatu jioni, ndege za kijeshi za Israel zilishambulia sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria na kuuwa shahidi washauri saba wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kilichoitishwa kujadili shambulio la utawala wa Israel kwenye sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria, Mohamed Khaled Khiari, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Mashariki ya Kati, Asia na Pasifiki amesema kwamba usalama wa majengo ya kidiplomasia na kibalozi na wafanyakazi wake lazima ulindwe katika hali zote kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa: "Mahesabu yoyote mabaya yanaweza kusababisha mzozo mkubwa zaidi katika eneo la Magharibi mwa Asia na matokeo mabaya kwa raia ambao kwa sasa wanakumbwa na mateso yasiyo na kifani huko Syria, Lebanon, maeneo ya Palestina na Mashariki ya Kati."Zahra Ershadi, balozi na naibu mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa alisema katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba utawala wa Israel umekiukaji waziwazi Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa, uhuru na mamlaka ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria; na Tehran inalinda haki yake ya kujibu uhalifu huo.

Katika mkutano huo wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wawakilishi wengi waliohudhuria wamelaani shambulizi hilo, wakilitaja kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na kwamba litakuwa sababu ya kuongezeka mvutano katika kanda hiyo. Wawakilishi wa nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Russia, China, Misri, Uswisi, Qatar na Uturuki, wameitaja hatua hiyo ya Israel kuwa ni ukiukaji mkubwa wa Mkataba wa Vienna wa 1968, ambao unatoa kinga kwa vituo vya kidiplomasia. Ingawa aghalabu ya wawakilishi walioshiriki katika kikao hicho cha UN wamelaani kitendo cha uchokozi cha Israel, lakini nchi chache ambazo ni waungaji mkono wa jadi wa jinai za Israel zikiwemo Marekani, Uingereza na Ufaransa, zimekataa kulaani mashambulizi ya utawala huo ghasibu  dhidi ya sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus. Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amedai katika mkutano huo kwamba bado hawajapata taarifa za kina kuhusu jengo lililoshambuliwa. Matamshi haya ya Marekani, hayawezi kuaminika wala kukubaliwa hasa kwa nchi hiyo inayojigamba kuwa na taarifa za moja kwa moja za matukio mbalimbali ya dunia.

Kukaa kimya waungaji mkono wa Kimagharibi wa Israel hususan Marekani dhidi ya jinai zinazofanywa na utawala huo ghasibu si suala geni, kwani jinai ya Wazayuni ya kushambulia ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria haikuwa ya kwanza na wala haitakuwa ya mwisho ya utawala huo ghasibu. Tangu tarehe 7 Oktoba ilipoanza duru mpya ya mashambulio ya Israel katika ardhi za Palestina hususan Gaza hadi sasa, utawala wa Kizayuni umekuwa ukilenga maeneo ya Syria Lebanon, ukiwemo uwanja wa ndege wa Damascus ambao ni lango la misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kwa Wapalestina, kwa kisingizio cha kulenga kambi ya Muqawama na mapambano.Mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria ni dharau ya wazi kwa kanuni inayokubaliwa na jamii ya kimataifa, yaani kinga ya wawakilishi wa nchi na maeneo ya kidiplomasia na ya kibalozi ambayo ni msingi wa mahusiano ya kimataifa. Wakati wa mashambulizi hayo pia, ambayo yamefanyika huku Israel ikikabiliwa na mashinikizo ya kimataifa ya kusitisha vita huko Gaza, unaonyesha upuuzaji wa makusudi wa wito wa kimataifa wa kusitisha mapigano.

 Ni wazi kuwa, lengo la hatua hiyo ya Israel ni kuliingiza eneo zima la Magharibi mwa Asia katika migogoro na vita, na inaonyesha hisia ya watawala wa Tel Aviv ya kulindwa na kukingiwa kifua na Marekani na nchi kadhaa za Magharibi na hivyo kujiona kuwa iko juu ya sheria za kimataifa. Kwa sababu hiyo, katika kipindi hiki muhimu, Baraza la Usalama linapaswa kuchukua msimamo madhubuti wa kuziwajibisha nchi na utawala huo ghasibu kuhusiana na udharura wa kuheshimu mamlaka na maeneo ya kidiplomasia. Pamoja na hayo yote na licha ya kuthibitika kwa walimwengu kwamba utawala mtendajinai wa Israel haujali wala kuheshimu kanuni, mikataba ya kimataifa na misingi ya kibinadamu na kimaadili, lakini inapaswa kueleweka kuwa wahusika na waungaji mkono wa jinai hiyo kubwa wataadhibiwa na Mujahidina na kambi ya Muqawama. Vilevile ieleweke kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kama ilivyotangaza, inahifadhi haki yake ya kujibu jinai hiyo mpya ya Wazayuni kwa wakati na mahali mwafaka. 

342/