Main Title

source : Parstoday
Jumatano

3 Aprili 2024

20:47:30
1448815

Rais Ebrahim Raisi: Israel iko kwenye sakaratul mauti, inakata roho

Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa, shambulio la juzi Jumatatu la utawala wa Kizayuni kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus Syria ni ushahidi kuwa Israel iko kwenye sakaratul mauti na inakata roho hivi sasa.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo katika mazungumzo ya simu aliyofanya jana usiku na Rais Bashar al Assad wa Syria na kuongeza kuwa, jinai iliyofanywa kwa mara ya kwanza na utawala wa kigaidi wa Israel ya kushambulia ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu si tu ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, lakini pia inaonesha ujuba wa kupitiliza wa Israel na jinsi utawala huo ulivyoporomoka kupindukia kimaadili sambamba na jinai kubwa unazozifanya katika nchi za Lebanon, Syria na Palestina.

Pia amesema, jinai hizo za utawala wa Kizayuni hasa huko Ghaza ni ushahidi kuwa Israel inapapatika katika hatua za mwisho za kukata roho hasa kwa kuzingatia kuwa leo hii kila mtu ameelewa kuwa utawala wa Kizayuni ni dola katili linalofanya unyama mkubwa dhidi ya wanawake na watoto. Kila mtu ameona jinsi Israel isivyojali sheria za kiimataifa na misingi ya ubinadamu.

Kwa upande wake Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa, jinai zinazoendelea kufanya na Israel huko Ghaza inalifanya ni jambo la dharura kwa kila mtu duniani kujitokeza na kuliunga mkono taifa la wanamuqawama la Palestina na kuhakikisha utawala wa Kizayuni unakomesha mara moja jinai zake.

342/