Siku ya Jumatatu, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zilifanya shambulio la anga lililolenga sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran katika Mtaa wa Al-Mazzah mjini Damascus, Syria.Kutokana na uchokozi huo, maafisa saba wa kidiplomasia na waambata wa kijeshi wa Iran waliuawa shahidi.Kwa mujibu wa IRNA, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema jana kuwa Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amelaani shambulio la Aprili Mosi dhidi ya vituo vya kidiplomasia vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus pamoja na vifo vilivyoripotiwa. Dujarric amefafanua kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza kwamba kanuni ya kinga ya majengo ya kidiplomasia na maafisa wa kibalozi lazima iheshimiwe katika hali zote kwa mujibu wa sheria za kimataifa.Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa vilevile anakumbusha pande zote kuheshimu majukumu yao yote chini ya sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na sheria za kimataifa za kibinadamu.
342/