Main Title

source : Parstoday
Jumatano

3 Aprili 2024

20:59:16
1448819

Salwan Momika, Muiraki aliyiivunjia heshima Qur'an mara kadhaa, aripotiwa kufariki akiwa Norway

Mkimbizi wa Iraq, Salwan Momika, ambaye alivunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu mara kadhaa mwaka jana, ameripotiwa kupatikana amefariki nchini Norway.

Kwa mujibu wa Press TV, Radio Genoa iliripoti katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X siku ya Jumanne kwamba mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 37 mwenye chuki dhidi ya Uislamu raia wa Iraq amepatikana amefariki.

Hata hivyo habari hii haijaweza kuthibitishwa rasmi na wakuu wa Norway.

"Wale waliotangaza kifo cha Momika walifuta ujumbe huo katika ukurasa wa X. Tunasubiri uthibitisho zaidi," ilisema Radio Geneo.

Momika, ambaye alipata umaarufu mkubwa duniani kwa kitendo chake cha kufuru cha kuchoma moto nakala ya Qur'ani, hivi karibuni alikimbilia Norway baada ya kutimuliwa Sweden au Uswidi.

Mnamo Juni 2023, Salwan Momika alikanyaga Qur'ani kabla ya kuteketeza moto kurasa zake kadhaa mbele ya msikiti mkubwa zaidi wa Stockholm. Kitendo hicho kiovu cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu kilifanywa chini ya idhini na ulinzi wa polisi wa Uswidi.

Tukio hilo lililosadifiana na siku kuu ya Idul al-Adha liliibua hasira za Waislamu kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kufuatia tukio hilo, mamilioni ya Waislamu katika nchi mbalimbali walijitokeza barabarani kulaani uchomaji moto wa matukufu ya Kiislamu nchini Uswidi.

342/