Main Title

source : Parstoday
Jumatano

3 Aprili 2024

21:00:36
1448822

Baraza la Usalama laitisha kikao cha dharura kuhusu shambulio la Israel kwenye ubalozi wa Iran

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha kikao cha dharura cha kujadili shambulizi la kigaidi la Israel katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus Syria kikao ambacho kimeshuhudia kulaaniwa vikali Israel kwa shambulio lake hilo la kigaidii.

Zahra Ershadi, Naibu Mwakilishi Maalumu wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa amelaani vikali jinai hizo za kutisha za kigaidi za Israel na kusema kuwa, utawala wa Kizayuni unakanyaga waziwazi sheria za kimataifa na haijali haki ya kujitawala nchi za Syria na Iran.

Nchi nyingine mbalimbali kama vile Russia nazo zimetumia hotuba zao kwenye kikao hicho kulaani vikali jinai hizo za kichokozi za Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kabla ya hapo pia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa naye alikuwa ametoa tamko la kulaani shambulizi hilo la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria na kuonya kwamba mahesabu yoyote ya kimakosa yanaweza kusababisha mapigano yenye wigo mpana zaidi katika eneo hili tete na lisilo na utulivu na kusababisha matokeo haribifu kwa raia.Siku ya Jumatatu, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zilifanya shambulio la anga lililolenga sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran katika Mtaa wa Al-Mazzah mjini Damascus, Syria. 

Kutokana na uchokozi huo, maafisa saba wa kidiplomasia na waambata wa kijeshi wa Iran wameuawa shahidi. Kwa mujibu wa IRNA, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema jana kuwa Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amelaani shambulio la Aprili Mosi dhidi ya vituo vya kidiplomasia vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus pamoja na vifo vilivyoripotiwa..

342/