Main Title

source : Parstoday
Jumatano

3 Aprili 2024

21:01:39
1448825

Muqawama wa Iraq: Tumeshambulia Haifa kulipiza kisasi cha jinai za Wazayuni Ghaza

Makukndi ya Muqawa wa Kiislamu ya Iraq yametangaza kuwa yameshambulia kambi ya jeshi la anga ya Tel Nof ya utawala wa Kizayuni kwenye mji wa Haifa ili kulipiza kisasi cha jinai zinazofanywa na Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Kwenye taarifa yake ya jana Jumanne, muqawama wa Iraq umesema kuwa, umeshambulia kwa droni kambi hiyo ya jeshi la anga la Israel ikiwa ni sehemu ya kupigana bega kwa bega na wanamapambano wa Palestina wanaokabiliana kiume na mashambulizi ya kila upande ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Makundi hayo ya mapambano ya Kiislamu ya Iraq yameongeza kuwa, yamekuwa yakifanya mashambulizi ya mfululizo kwa kutumia silaha zinazofaa kabisa dhidi ya maeneo ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ili kulipiza kisasi cha jinai za kuchupa mipaka zinazofanywa na utawala huo katili dhidi ya Wapalestina.Makundi hayo yameingia vitani kushambulia maeneo muhimu sana ya Israel baada ya utawala huo katili ambao unaungwa mkono kwa hali zote na Marekani na madola mengine ya kibeberu ya Magharibi, kuzidisha jinai zake dhidi ya wanawake na watoto wadogo pamoja na vizee na raia wa kawaida huko Palestina hasa Ghaza. Katika mikakati na stratijia zake mpya, kambi ya muqawama ya Iraq imeamua sasa kuzidisha mashambulizi yake dhidi ya maeneo muhimu sana ya utawala wa Kizayuni yakijumuisha pia viwanja vya ndege na kambi za kijeshi za Israel ili kuulazimisha utawala huo ukomeshe jinai zake dhidi ya Wapalestina.

342/