Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

4 Aprili 2024

14:17:48
1449043

Kufungwa kituo cha televisheni cha Al Jazeera Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel)

Radimali ya jinai za Israel dhidi ya watu wa Gaza katika vyombo vya habari vya dunia na wimbi la upinzani na lawama za kimataifa kuhusu jinai hizo zimeufanya utawala wa Kizayuni kufunga mara moja kituo cha Televisheni ya Al-Jazeera katika Ukanda wa Gaza kutokana na jinsi inavyoakisi habari za mauaji ya kimbari ya utawala huo katika vita hivyo.

Kuhusiana na jambo hilo, Bunge la Israel limepasisha na kuidhinisha mswada uliowasilishwa na Baraza la Mawaziri la Vita la Benjamin Netanyahu wa kufunga mara moja televisheni ya Al Jazeera katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel). Sambamba na kuidhinishwa sheria hiyo, Netanyahu ameandika katika ukurasa wake wa X kwamba: Wakati umefika wa kuifunga Al Jazeera." Ingawa sheria hiyo imepitishwa kuhusiana na Al Jazeera, lakini inampa Waziri wa Mawasiliano wa Israel kibali cha kubatilisha kibali cha chombo chochote cha kigeni baada ya kumkinaisha waziri mkuu kwamba matangazo yake yanahatarisha usalama wa utawala huo wa Kizayuni.Benjamin Netanyahu ameandika kuhusiana na suala hilo katika ukurasa wa X kwamba: Kanali ya kigaidi ya Al Jazeera haitatangaza tena matangazo yake kutoka Israel na nitachukua hatua za haraka kwa mujibu wa sheria mpya kukata kabisa shughuli za kanali hii. Kanali ya Televisheni ya Al Jazeera, inayomilikiwa na nchi ya Qatar, imekuwa na ofisi rasmi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kwa zaidi ya muongo mmoja na inatangaza matangazo yake kwa lugha za Kiarabu na Kiingereza. Katika miezi ya hivi karibuni Waandishi wengi wa habari na wasimamizi wa kanali hiyo wameuawa shahidi hasa katika vita vya Gaza. Kuhusiana na hilo, tunaweza kuashiria kuuawa shahidi Shirin Abu Aqleh, Samir Abu Daqeh, Hamza Al-Dahdouh  pamoja na kulipuliwa  ofisi ya kituo chicho cha habari huko Gaza.

Katika mahojiano na kituo cha  Al Jazeera, Irene Khan, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuhusu uhuru wa kujieleza: "Inashangaza kuona jinsi jeshi la Israel linavyoamiliana na waandishi wa habari wa Gaza."

Vitendo vya Israel dhidi ya waandishi wa habari huko Gaza vinakinzana wazi na sheria za kimataifa na hivyo sote tunalazimika kuchukua msimamo wa kuiwajibisha katika uwanja huo.

Tangu vita vya Gaza, kanali ya televisheni ya Al Jazeera imekuwa ikionyesha jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya wakaazi wa ukanda huo. Katika moja ya ripoti zake za hivi karibuni, kituo hicho kilifichua jinai za kutisha za Israel dhidi ya wanawake wa Kipalestina.

Ilisema: 'Wanajeshi wa Israel waliwabaka na kuwaua wanawake katika operesheni yao katika hospitali ya Shafa huko Gaza.'

Kwa hakika, kuakisiwa kwa mapana na marefu jinai za Israel dhidi ya Wapalestina na kuongezeka mashinikizo ya fikra za waliowengi duniani dhidi ya Israel kumewapalekea watawala wa Tel Aviv kufunga kabisa shughuli za kanali hiyo katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Kevin McCue, mkuu mtendaji wa shirika linalounga mkono uhuru wa vyombo vya habari, anasema kuhusiana na hili: 'Kuzuia upashaji habari wa wakala wa habari wa kutegemewa kama Al Jazeera kamwe hakupaswi kupuuzwa. Hii ni hatua ya kusikitisha sana kupoteza chanzo muhimu cha upashaji habari kinachoaminika.'