Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

4 Aprili 2024

14:18:27
1449044

SEPAH: Magaidi 15 wameshaangamizwa hadi hivi sasa kusini mashariki mwa Iran

Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesema kuwa, hadi hivi sasa magaidi 15 wameshaangamizwa katika operesheni za kuzima mashambulizi matatu ya kigaidi yaliyofanywa na magaidi hao kusini mashariki mwa Iran.

Genge la kigaidi la "Jaish al Dhulm" linaloungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, jana usiku lilifanya mashambulizi ya kigaidi kwa wakati mmoja katika vituo mbalimbali vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH katika miji ya Rask na Chabahar, kusini mashariki mwa Iran, lakini mashambulizi yote hayo yamezimwa na vikosi vya kulinda usalama wa taifa la Iran tangu mwanzoni kabisa kwa kuanza kwake. 

Shirika la habari la Iran Press limemnukuu Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour, Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la SEPAH akisema hayo leo Alkhamisi na kuongeza kuwa, magaidi walioshiriki kwenye uvamizi huo wote walikuwa wamevaa vizibao vya kujiripua kwa mabomu na kuna uwezekano idadi ya magaidi walioangamizwa ikaongezeka. Ameongeza kuwa, huko Chabahar, vituo viwili vya Jeshi la SEPAH vimeshambuliwa na magaidi hao na lengo la genge hilo la kigaidi ni kwamba kwanza wawaue walinzi wa mlangoni lakini hapo hapo waliangamizwa magaidi watano na kuzimwa mashambulizi yao. Pia amesema, watu wote waliokuwa wametekwa nyara na magaidi hao wamekombolewa baada ya wanajeshi wa SEPAH kuingia na hivi sasa vikosi maalumu vya jeshi hilo la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu vinaendesha operesheni za kusafisha kikamilifu mabaki ya magaidi hao. Amesema, utulivu na usalama umesharejea kwenye hali yake ya kawaida ya kabla ya uvamizi wa magaidi hao wa jana usiku huko Rask na Chabahar. 

342/