Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

4 Aprili 2024

14:19:21
1449046

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akosoa upuuzaji wa Umoja wa Ulaya kuhusu ugaidi wa Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa misimamo ya undumakuwili ya Umoja wa Ulaya na upuuzaji wake kuhusiana na jinai na vitendo vya kigaidi vya utawala ghasibu wa Israel.

Siku ya Jumatatu Aprili 1, 2024, ndege za kivita za Israel zilishambulia ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus. Watu kumi na watatu wakiwemo wanachama saba wa vikosi vya kidiplomasia na kijeshi vya Iran waliuawa shahidi katika shambulio hilo la kigaidi.

Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika mazungumzo yake na Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni na Usalama wa Umoja wa Ulaya amesema viongozi wa Ulaya daima wanaitaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa na subira inapochikozwa katika hali ambayo utawala wa Israel, unaokiuka wazi sheria na kanuni za kimataifa, umeshambulia sehemu ya kidiplomasia ambayo ina kinga kamili kwa kuzingatia Mkataba wa Haki za Kidiplomasia na Kibalozi.

Amesema, mauaji ya kimbari na jinai za kivita zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel zinaendelea huko Ghaza kwa uungaji mkono kamili wa Marekani, na bila ya kuwepo irada kubwa ya Washington ya kudhibiti na kuacha kuunga mkono jinai za kivita za utawala huo.

Amir Abdollahian akisisitiza kuwa shambulio la utawala wa Kizayuni katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanafanya kazi nchini Syria wakiwa na hati za kusafiria za kidiplomasia kwa mwaliko rasmi wa serikali ya Syria kwa ajili ya kuisaidfia kupambana na ugaidi.

Amesisitiza kwamba utawala wa Kizayuni unapaswa kuadhibiwa katika mfumo wa sheria za kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aidha katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon, Abdallah Bouhabib amesema: Kwa kuzingatia uungaji mkono wa pande zote kwa jinai za utawala wa Kizayuni, Marekani inapaswa kuwajibishwa kutokana na hatua za kichokozi na za kigaidi za utawala huo ghasibu.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Lebanon amesema: Lebanon inakubaliana na Iran kuhusiana na ulazima wa kusimamishwa vita katika Ukanda wa Gaza na kutohatarishwa amani katika eneo na dunia.

342/