Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

4 Aprili 2024

14:19:58
1449047

Shambulio la kigaidi kusini mashariki mwa Iran

Alireza Marhamati, Naibu Gavana anayesimamia masuala ya usalama na utekelezaji sheria katika mkoa wa Sistan na Baluchistan, kusini mashariki mwa Iran, ametangaza kutokea shambulio la kigaidi kwenye makao makuu mawili ya kijeshi katika miji ya Rask na Chabahar mkoni humo.

Kundi la kigaidi la Jaish al-Dhulm, ambalo lina mafungamano na utawala wa Kizayuni Jumatano usiku, lilijaribu kuteka makao makuu ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC huko Rask na Chabahar.

Alireza Marhamati amesema kuwa hali katika eneo hilo iko chini ya udhibiti wa vikosi vya usalama vya Iran.

Akifafanua kuhusu shambulio hilo la kigaidi katika mkoa wa Sistan na Baluchistan amesema magaidi wa Jaish al-Dhulm ambao wana mafungamano na Wazayuni hawakufanikiwa kuyateka makao makuu ya IRGC huko Chabahar na Rask na kwamba wamezingirwa na vikosi vya usalama.

Amesema, operesheni za magaidi hao katika maeneo ya Chabahar na Rask zimeshindwa kutokana na makabiliano ya vyombo vya ulinzi na usalama na kufafanua kuwa magaidi wanne wamezingirwa na vyombo vya usalama na raia mmoja amechukuliwa mateka ambapo juhudi za kumuokoa zinaendelea.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, askari watano wa kulinda usalama wa Iran wameuawa shahidi na magaidi watano pia kuangamizwa katika mashambulizi hayo ya kigaidi yaliyotokea kusini mwa Sistan na Baluchestan. Wakazi wa mkoa huo wana kumbukumbu chungu za uadui na jinai za watumishi na mamluki wa madola ya kibeberu tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, lakini pamoja na hayo hawajawahi kuvunjika moyo katika azma yao thabiti ya kulinda usalama wa nchi yao na mafanikio ya mfumo wa Kiislamu. Tangu takriban miaka 17 iliyopita, wakazi wa Kishia na Kisunni wa mkoa huo wameandikisha kumbukumbu chungu ya jinai za makundi ya kigaidi katika kitabu cha ushujaa na uthabiti wao.
Matukio mengi ya jinai yalianza pale mhalifu aliyeitwa "Abd al-Malik Rigi" pamoja na kundi lake la "Jund al-Shaitan" alipofanya jinai za kutisha na za woga dhidi ya watu wasio na hatia wa mkoa huo kwa ajili ya kuwatumikia mabwana zake wa kibeberu na makatili. Baada ya kutiwa mbaroni na kuangamizwa Abdul Malik Rigi, kaka yake Abdul Hamid na baadhi ya viongozi wa kundi la Jund al-Shaitan nchini Iran na Pakistan, mabaki ya kundi hilo la kigaidi yameendelea kufanya jinai katika mfumo wa Jaish al-Dhulm lenye uhusiano na al-Qaeda katika pembe tofauti za mkoa wa Sistan na Baluchistan, yakitokea katika ardhi ya Pakistan.

342/