Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

4 Aprili 2024

14:21:34
1449050

Viongozi wa Kiislamu Marekani wakataa mwaliko wa Biden wa Futari kutokana na ukatili wa Israel huko Gaza

Rais Joe Biden wa Marekani amelazimika kuandaa karamu ndogo Futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Ikulu ya White House baada ya idadi kubwa ya viongozi wa Kiislamu kukataa mwaliko wake kutokana na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala haramu wa Israel unaotenda ukatili katika Ukanda wa Gaza.

Ikulu ya White House hapo awali ilialika kundi la viongozi wengi wa jumuiya za Kiislamu kwa dhifa ya Futari

Lakini hafla hiyo imegonga mwamba baada ya viongozi wengi kukataa kula chakula meza moja na Biden na Makamu wake, Kamala Harris Jumanne jioni.

Ikulu ya White ililazimika kuandaa hafla ndogo ambayo ilihudhuriwa na Harris, Mshauri wa Usalama wa Taifa, Jake Sullivan, wasaidizi wakuu wa Ikulu ya White House na chini ya watu kumi na wawili wanaofanya kazi serikalini.

Kwa mujibu wa Wa’el Alzayat, anayeongoza shirika la kutetea Waislamu la Emgage, viongozi wa Kiislamu walikataa mwaliko wa Biden, wakiamini kwamba siku moja haitoshi kujiandaa kwa fursa ya kugeuza mawazo ya Biden kuhusu uungaji mkono wake kwa ukatili wa Israel huko Gaza. Amesema “Haifai kushiriki katika dhifa kama hiyo huku kukiwa na njaa huko Gaza.”

Salima Suswell, kiongozi wa Baraza la Uongozi la Waislamu Weusi, ameliambia gazeti la Washington Post kwamba yeye na viongozi wengine wa Kiislamu walialikwa kwenye chakula cha jioni katika Ikulu ya White House lakini walikataa mwaliko kama njia ya kutangaza uungajii mkono wao kwa Wapalestina.

Nihad Awad, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR), amewahimiza viongozi wengine wa Kiislamu kukataa mialiko ya kwenda Ikulu ya Marekani iwapo wataipokea.

342/