Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

5 Aprili 2024

14:46:51
1449243

Siku ya Kimataifa ya Quds; Siku ya mwamko wa Ulimwengu wa Kiislamu

Leo Ijumaa tarehe 5 mwezi Aprili inayosadifiana na tarehe 25 Ramadhani 1445 hijria shamsia ni Siku ya Kimataifa ya Quds.

Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kufuatia ubunifu wa Imam Khomeini (RA), mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Taifa la Kiislamu la Iran linalitazama suala la Palestina kama kadhia ya dharura katika kuyaunga mkono mataifa yanayodhulumiwa na yanayokabiliwa na ukandamizaji wa mabeberu baada ya kutangazwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Suala la Palestina ni kadhia kuu inayouhusu Ulimwengu wa Kiislamu na haipasi kupuuzwa wakati wowote; kwa msingi huo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa kinara katika kuyaunga mkono mataifa madhulumu duniani, inaamini kuwa kuwaunga mkono wananchi  madhulumu wa Palestina ni suala kuu la ulimwengu wa  Kiislamu, na kusisitiza juu ya haki ya msingi ya Wapalestina ya kujianishia mustakbali wao na kuwa wamiliki wakuu wa ardhi hizo zilizoghusubiwa na utawala haramu wa Israel. 

Kwa msingi huo, Siku ya Kimataifa ya Quds si tu ni harakati ya kulaani uvamizi huo, bali pia ni ishara ya mwamko wa Umma wa Kiislamu dhidi ya njama mbalimbali za uistikbari zinazoongozwa na Marekani, Israel na waitifaki wao katika eneo. Waislamu walioko katika saumu nchini Iran na katika nchi nyingine za Kiislamu leo Ijumaa wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Ukanda wa Gaza dhidi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni. 

342/