Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

5 Aprili 2024

14:47:20
1449244

Wanajeshi wa Israel wazuiliwa kwenda livu ya nyumbani kwa tahadhari na hofu ya shambulio la Iran

Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limesitisha livu ya nyumbani kwa wanajeshi wake kutokana na kuwepo hofu inayoongezeka ya utawala huo kuandamwa na shambulio la kulipiza kisasi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iran kufuatia shambulio la kigaidi ulilofanya wiki hii kwenye ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria.

 Taarifa iliyotolewa na jeshi la Kizayuni IDF imesema, kulingana na tathmini ya hali ya mambo, imeamuliwa kuwa likizo itasitishwa kwa muda, kwa vitengo vyote vya kivita vya jeshi hilo. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, jeshi hilo liko vitani na suala la kutumwa vikosi kwenye medani ya mapigano linapitiwa mara kwa mara inapohitajika. Itakumbukwa kuwa maafisa wa saba wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC wakiwemo majenerali wawili wakuu, waliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi lililofanywa  na utawala wa Kizayuni dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus siku ya Jumatatu.Iran imeishutumu Israel kwa kutekeleza shambulizi hilo na kuahidi kujibu mapigo.

 Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya utawala haramu wa Israel, mamlaka mjini Tel Aviv zinafikiria kufungua makazi ya maficho kufuatia kitisho ilichotoa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran cha kulipiza kisasi. Siku ya Jumatano, jeshi la utawala wa Kizayuni liliamua kuwaita wanajeshi wa akiba kwenye safu yake ya ulinzi ya anga, katika hatua iliyotajwa na vyombo vya habari vya ndani kama hatua ya tahadhari dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya kulipiza kisasi yatakayofanywa na Iran.../


342/