Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

5 Aprili 2024

14:48:25
1449245

Kamanda Mkuu wa IRGC: Israel inakaribia kusambaratika

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) anasema utawala wa Kizayuni wa Israel utasambaratika hivi karibuni, akibainisha kuwa Marekani inaiunga mkono waziwazi Israel.

Meja Jenerali Hossein Salami aliyasema hayo leo Ijumaa alipokuwa akiwahutubia mamilioni ya Wairani mjini Tehran waliojitokeza mabarabarani kuonesha mshikamano na Wapalestina na kulaani ukatili unaofanywa na Israel kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds.

Kamanda Mkuu wa IRGC ameongeza kuwa: â€œUtawala wa Kizayuni ni jambia ambalo utawala wenye uovu na wenye kuhadaa wa Uingereza ulilipenyeza kwenye mwili wa Umma wa Kiislamu miaka 75 iliyopita. Baada ya hapo utawala utendao uhalifu wa Marekani umeupa ujasiri utawala huo na kuutumia kama chombo cha kisiasa, kiusalama na kijiografia katika ulimwengu wa Kiislamu ili kueneza satwa yake."

Aliendelea kuitaja Israel kuwa ni utawala bandia unaotumikia sera mbovu za baadhi ya nchi za Magharibi, na kusisitiza kwamba jinai zisizohesabika za utawala huo ghasibu zimevuruga usalama wa Palestina na mataifa mengine ya Kiarabu na Kiislamu.Kamanda huyo wa IRGC aliendelea kusema kuwa Israel, ikiungwa mkono na Marekani, Uingereza na Ufaransa, ilianzisha vita ili kuwafukuza kwa nguvu Wapalestina kutoka katika nchi yao. Ameongeza kuwa, Wazayuni na waungaji mkono wao wa Marekani wanaamini kadiri wanavyowaua Waislamu na kuwazingira na kuwalazimisha kuyahama makazi yao, ndivyo wanavyoweza kuishi vizuri zaidi. Amesema ukweli ni kinyume na wanavyodhania.
 Kamanda Mkuu wa IRGC amesema hivi sasa "Utawala wa Kizayuni unahangaika kwani uko katika hali ya baina ya maisha na kifo na kwamba hatima ya utawala huo ni kushindwa bila kujali iwapo utendeleza au kusitisha vita Gaza. Kwingineko katika matamshi yake, Salami aliionya Israel kwamba bila shaka itapata jibu kwa shambulio la makombora dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria.
 Akiashiria matamshi yaliyotolewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei, jenerali huyo amesema majeshi ya Iran yataiadhibu Israel.

342/