Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

5 Aprili 2024

14:52:35
1449248

Washiriki wa matembezi ya Siku ya Quds Iran: Jibu kali na la kujutisha umeandaliwa utawala wa Kizayuni

Washiriki wa matembezi ya Siku ya Quds Duniani yaliyofanyika mjini Tehran wamesisitiza katika azimio walilotoa mwishoni mwa matembezi hayo juu ya kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Ghaza na wakalaani jinai ya utawala bandia wa Kizayuni ya kushambulia balozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Syria.

Washiriki hao wa matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds wamesisitiza kwamba, jibu kali na la kujutisha limeandaliwa kwa ajili ya utawala wa Kizayuni Leo Ijumaa tarehe 5 Aprili 2024 inayosadifiana na mwezi 25 Ramadhani 1445 ni Siku ya Quds Duniani. Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa kwa ubunifu wa Imam Khomeini (RA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Baada ya kutangazwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds, Umma wa Kiislamu unaitazama kadhia ya Palestina suala la dharura na lenye ulazima katika kuyaunga mkono mataifa yanayodhulumiwa na yanayonyongeshwa. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, matembezi ya Siku ya Quds Duniani yamefanyika kote nchini Iran leo Ijumaa katika miji na vijiji zaidi ya elfu mbili ikiwemo miji mikubwa ya Tehran,
 
Mashhad, Qom, Esfahan na Shiraz.
Katika azimio walilotoa mwishoni mwa matembezi hayo, washiriki wa matembezi ya Siku ya Quds Duniani wamelaani na kuonesha walivyochukizwa na jinai za adui Mzayuni na wakatangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na kueleza kwamba: mapigano ya Kimbunga cha Al-Aqsa na kuendelea Muqawama wa watu wa Ukanda wa Ghaza na Mujahidina wa Palestina kwa siku 183 ni nukta ya mabadiliko makubwa katika mapambano dhidi ya uwepo wa utawala khabithi na bandia wa Kizayuni; na mapigano hayo yameongeza kasi na kukaribia zaidi lahadha ya kuangamizwa na kutokomezwa dondandugu la saratani la Israel katika jiografia ya Ulimwengu wa Kiislamu.Sehemu nyingine ya azimio hilo imeeleza kwamba, washiriki wa matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds wanaipa indhari Marekani, -ambayo ndiyo mtuhumiwa wa kwanza wa uendeshaji vita vya Ghaza na muungaji mkono bila masharti yoyote wa Wazayuni-, kwamba ijiepushe na kulipa gharama zaidi za kistratijia na za kufedhehesha zinazotokana na kushindwa na kushiriki katika jinai na mauaji ya kimbari katika Asia Magharibi na kuitafakari upya sera yake ya kishetani, ili isizidi kuichafua na kuiporomosha heshimu ya watu wa Marekani kwa sababu ya kuwaunga mkono wauaji wa wanawake na watoto wa Ghaza.

Halikadhalika, katika azimio la mwishoni mwa matembezi ya Siku ya Quds Duniani, washiriki wamelaani minong'ono inayosikika ya kuendelezwa mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala bandia na ghasibu wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu na wakasisitiza kwamba, serikali za nchi hizo zinapaswa kukidhi matakwa ya wananchi wao kwa kuuwekea vikwazo na kuukatia mirija ya uchumi utawala katili wa Kizayuni muuaji wa watoto na kuwasaidia wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina na Ghaza ili waweze kuondokana na shari ya jinai na masaibu yanayowaandama hivi sasa na kufanya juhudi zao zote kwa ajili ya kuhakikisha usitishaji vita wa kudumu unatekelezwa katika Ukanda wa Ghaza.../

342/