Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Aprili 2024

14:36:14
1449774

Wanamuqawama wa Iraq washambulia eneo muhimu la Israel katika kuunga mkono Gaza

Harakati ya Muqawama (mapambano ya Kiislamu) nchini Iraq imetekeleza kwa mafanikio shambulio la ndege zisizo na rubani dhidi ya maeneo ya kistratijia katika sehemu ya kusini kabisa ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina bandia la Israel. Hujuma hiyo imetekelezwa ili kukabiliana na mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza.

Harakati ya Muqawama ya Iraq, kundi mwavuli la wapiganaji wa kupambana na ugaidi, katika taarifa iliyochapishwa kwenye kituo chake cha Telegram, imetangaza kuhusika  na shambulio dhidi ya eneo "muhimu" katika bandari ya Eilat, ambayo iko kwenye ncha ya kaskazini ya Bahari ya Sham.

Taarifa hiyo imebaini kuwa shambulio hilo la Jumapili ambalo lilitekelezwa kwa  ndege zisizo na rubani lilifanyika katika kuendeleza mapambano dhidi ya utawala ghasibu Israel, na kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza, hasa kwa ajili ya kulipiza kisasi mauaji yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wanawake, watoto na wazee katika eneo hilo linalozingirwa.

Harakati ya Muqawama ya Iraq imesisitiza kuwa itaendelea kulenga na kuharibu maeneo muhimu ya utawala wa Israel.

Hapo awali Harakati ya Muqawama ya Iraq ilitangaza kuwa ilikuwa ikilenga vinu vya kusafisha mafuta vya Haifa kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Katika mikakati na stratijia zake mpya, kambi ya muqawama ya Iraq imeamua sasa kuzidisha mashambulizi yake dhidi ya maeneo muhimu zaidi ya utawala wa Kizayuni yakijumuisha pia viwanja vya ndege na kambi za kijeshi za Israel ili kuulazimisha utawala huo ukomeshe jinai zake dhidi ya Wapalestina.

Utawala haramu wa Israel ulianzisha mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Ukanda wa Gaza, yakilenga hospitali, makazi na nyumba za ibada, tangu harakati za muqawama wa Palestina zilipoanzisha mashambulizi ya kushtukiza yaliyopewa jina la Operesheni ya al-Aqsa Dhoruba dhidi ya utawala huo ghasibu tarehe 7 Oktoba.

Tokea wakati huo jeshi katili la Israel limeua takriban Wapalestina 33,173, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Watu wengine 75,815 wamejeruhiwa pia na hawawezi kupata matibani baada ya Israel kubomoa karibu hospital izote Gaza.