Kwa mujibu wa Mtandao wa Habari wa Muqawama katika Telegram, askari hao wa Kizayuni waliangamizwa jana Jumamosi kwenye msururu wa mashambulizi ya kuvizia yaliyofanywa na tawi la kijeshi la Hamas la Izzuddinul-Qassam katika mji wa Khan Younis. Mashambulizi yaliyoratibiwa kwa umakini zaidi yalifanyika dhidi ya vikosi vya Kizayuni katika kitongoji cha al-Zana na kupelekea kuangamizwa askari tisa. Kwa mujibu wa chaneli hiyo ya habari, operesheni hiyo ilishuhudia wapiganaji wa Kipalestina wakivilenga vifaru vitatu vya Merkava moja kwa moja, na kisha kuwazingira na kuwashambulia kwa vifaa vitatu vya miripuko askari waliokuja kujaribu kuwaokoa wale waliokuwa wamejeruhiwa katika shambulio la kwanza."Vikosi vya uokoaji vililengwa tena saa chache baadaye, pamoja na wale waliokimbilia nyumba iliyo karibu," imeeleza chaneli hiyo ya habari ya Muqawama wa Palestina.
342/