Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Aprili 2024

14:38:01
1449776

Mashinikizo ya kusitisha uuzaji silaha kwa Israel yaongezeka katika nchi za Magharibi

Wabunge na maafisa wa serikali za nchi za Magharibi wanaendelea kutoa wito wa kusitishwa uuzaji wa silaha kwa Israel kutokana na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza kwa muda wa miezi 6, ambayo hadi sasa yameua shahidi Wapalestina zaidi ya 33,000 na kujeruhi wengine zaidi 75,000 tangu Oktoba 7 mwaka jana.

Nchini Ufaransa, wabunge 115 wametuma barua kwa Rais Emmanuel Macron wakimtaka kusitisha mauzo yote ya silaha kwa utawala katili wa Israel na kuonya kwamba, kutochukua hatua hiyo kunaifanya Ufaransa kuwa mshirika katika mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina.

Wabunge hao wamesema kuwa, kusitisha uuzaji wa aina zote za silaha kwa serikali ya misimamo mikali ya mrengo wa kulia ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kutaimarisha juhudi za amani katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Wabunge hao wamemtaka Macron kuiga mfano wa nchi nyingine kama Canada na Uholanzi ambazo zimechukua maamuzi wa kupiga marufuku uuzaji wa silaha kwa Israel kutokana na mauaji yanayofanyika Ukanda wa Gaza.

Katika barua yao, wabunge hao wamemkumbusha Rais wa Ufaransa kwamba idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza itazidi 33,000 katika siku zijazo. Vilevile wamemkumbusha kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Haki mwezi Januari mwaka huu iliamua kwamba kulikuwa na hatari ya mauaji ya kimbari huko Gaza, na kuitaka Israel kuzuia jambo hilo.

Nchini Ujerumani pia, kundi la mawakili na wanasheria lilitangaza Ijumaa iliyopita, kufungua kesi ya dharura dhidi ya serikali ya Ujerumani ili kuilazimisha isitishe mauzo ya silaha kwa Israel, kwa tuhuma kwamba silaha hizo "zinatumika katika ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.”

Hii ni kesi ya pili kuwasilishwa na mawakili hao mahakamani dhidi ya serikali ya Ujerumani.

Katika mashtaka yao, wanasheria hao wmetegemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kwamba Ujerumani imekuwa mmtoaji msaada mkubwa zaidi wa silaha wa Ulaya kwa utawala katili wa Israel, na kwamba thamani ya silaha za Ujerumani zilizopelekwa Israel ilifikia takriban euro milioni 326 mwaka 2023, nyingi zikiwa baada ya Oktoba 7, ambapo Ujerumani iliongeza mauzo ya silaha kwa Israel kwa takriban mara 10.Wakati huo huo, Ijumaa wiki hii, mbunge na spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, alitia saini barua iliyotumwa kwa Rais Joe Biden na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Anthony Blinken, akitaka kusitishwa operesheni za kupeleka silaha kwa utawala wa Isarel. Barua hiyo ilitiwa saini na wawakilishi 40 wa chama cha Democratic,
na kusema: "Kwa kuzingatia mauaji ya hivi majuzi ya wafanyikazi wa misaada ya kibinadamu na hali mbaya ya watu wa Gaza, tunaamini kuwa sio haki kuidhinisha utumaji wa silaha huko Israel." Itakumbukwa pia kwamba, juzi Ijumaa, Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kupiga marufuku usafirishaji wa silaha kwenda Israel kutokana na kuendelea vita vya utawala huo ghasibu dhidi ya watu Ukanda wa Gaza. Huu ni msimamo wa kwanza kuchukuliwa na baraza hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu vita dhidi ya Gaza.

342/