Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Aprili 2024

14:40:17
1449779

Jenerali Baqeri: Shambulio la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria lilikuwa 'kujiua'

Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran amesema shambulizi la hivi karibuni la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya vituo vya kidiplomasia vya Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus, ni sawa na kichaa na kujitia kitanzi utawala huo.

Meja Jenerali Mohammad Baqeri, Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Iran ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika shughuli ya mazishi ya Meja Jenerali Mohammad Reza Zahedi katika mji wa Isfahan jana Jumamosi, huku umati wa watu kwenye mkusanyiko huo ukipiga nara za "mauti kwa Israel" na "mauti kwa Marekani".

Zahedi alikuwa miongoni mwa washauri saba wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) waliouawa shahidi katika shambulizi la anga la Israel lililolenga sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran katika kitongoji cha Mezzeh mjini Damascus, Jumatatu iliyopita.

"Shambulio la hivi karibuni la makombora kwenye jengo la ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus, eneo lenye kinga ya kimataifa, ni aina ya wendawazimu na linaashiria kujitia kitanzi kwa utawala wa Kizayuni," Baqeri amesema.

Akisisitiza kwamba, shambulizi la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran lilitokana na kukata tamaa kwa utawala wa Kizayuni, Meja Jenerali Baqeri, ameongeza kuwa: "Tutamwadhibu adui kwa msaada wa watu wetu mashujaa na tutalipiza kisasi."

Afisa huyo wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran amesisitiza kuwa, "Tumejifunza kutoka kwa makamanda wetu wakubwa kuamua wakati, aina na mpango wa operesheni, na hili litafanywa kwa wakati unaofaa na kwa uharibifu mkubwa kwa adui."

Baqeri pia ameonya kwamba, Marekani ndiyo iliyobeba jukumu kuu la shambulio hilo, na Washington lazima iwajibishwe.

Tarehe Mosi Aprili ndege za kivita za Israel zilishambulia kwa makombora sita ubalozi mdogo wa Iran, katika wilaya ya Mezzeh mjini Damascus.

Zahedi, kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC nchini Syria an Lebanon, na naibu wake, Jenerali Mohammad Hadi Haji Rahimi waliuawa shahidi katika shambulio hilo la kigaidi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alisema siku ya Jumatano kwamba Israel itazabwa kibao cha uso kwa muaji hayo.

342/