Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Aprili 2024

14:42:09
1449782

Kwa miongo saba, Marekani imeipatia Israel msaada wa dola bilioni 300

Jopo la wanafikra la Baraza la Uhusiano wa Nje la Marekani limetoa ripoti kuhusu kiwango cha msaada wa karibu dola bilioni 300 ambazo Washington, ikiwa ndiye muungaji mkono mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, imetoa katika muda wa miongo saba kuupatia utawala huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Anatolia, data za Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani ambazo zimetumiwa kwenye ripoti ya Baraza la Uhusiano wa Nje zimeonyesha kuwa, "tangu ilipoasisiwa hadi mwaka 2023, Israel imekuwa ndiye mpokeaji mkubwa zaidi wa misaada ya nje ya Marekani, na kwamba jumla ya misaada ya kijeshi na kiuchumi iliyopokea kutoka serikali ya Washington inafikia takriban dola bilioni 300". Katika ripoti hiyo, imeandikwa kwamba misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Tel Aviv baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya tarehe 7 Oktoba 2023 na mashambulizi yaliyofuata ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza, ambayo yamepelekea makumi ya maelfu ya watu kuuawa shahidi katika eneo hilo, imekabiliwa na ukosoaji mwingi na kuwa mada ya mjadala mkali katika ngazi ya kimataifa.

Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti hiyo, Marekani imetoa msaada mkubwa wa kiuchumi kuupatia utawala wa Kizayuni kati ya mwaka 1971 na 2007.

 Marekani imekuwa ikikosolewa vikali kutokana na utoaji misaada hiyo ya kijeshi na kuupatia silaha utawala wa Kizayuni, kutokana na ukweli kwamba mashambulizi ya utawala huo katika Ukanda wa Ghaza yamepelekea kuuawa raia. Hivi karibuni, gazeti la Marekani la Washington Post liliripoti kuwa  kwa kutumia "mamlaka ya hali ya dharura" utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani, umetangaza hadharani miamala miwili tu kati ya zaidi ya miamala 100 ya silaha na vifaa vya kijeshi iliyofanya na utawala wa Kizayuni tangu Oktoba 7, 2023.  Gazeti la Washington Post limefichua pia kwamba hivi karibuni serikali ya Marekani iliidhinisha kuuuzia utawala wa Kizayuni ndege 25 za kivita aina ya F-35 na injini za ndege, pamoja na mabomu 1,800 aina ya MK84 na 500 MK82  lakini haikutangaza hadharani. Kwa muda wa miezi sita sasa, Israel imekuwa ikifanya kila aina ya jinai za kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ghaza, kwa uungaji mkono wa kisiasa na kijeshi wa Marekani, na hadi sasa imashawaua shahidi zaidi ya watu 33,000 wakiwemo watoto, wanawake na wazee.../


342/