Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Aprili 2024

14:42:46
1449783

Griffiths: Vita vinavyoendelea Ghaza kwa miezi sita sasa ni usaliti dhidi ya ubinadamu

Mratibu mkuu wa misaada na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema vita vinavyoendelea Ghaza vimefikia hatua ya kutisha.

Kupitia taarifa yake iliyotolewa mjini New York kwa mnasaba wa kutimia miezi sita ya vita hivyo Griffiths amesema “kwa watu wa Ghaza, miezi sita iliyopita ya vita imeleta vifo, uharibifu na sasa matarajio ya aibu ya njaa iliyosababishwa na mwanadamu.”

Mratibu mkuu wa misaada na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa ameendelea kueleza kwamba, “kila siku, vita hivi vinaongeza idadi ya waathirika waliopoteza maisha miongoni mwa raia. Kila sekunde vita vinapoendelea vinapanda mbegu za mustakbali uliogubikwa na vita hivyo visivyokoma.” 

Griffiths amebainisha kuwa, yeye na wengine wengi wamesema mara kwa mara kwamba mwisho wa vita vya Ghaza umechelewa sana, na sasa ni wakati wa kuvikomesha.Ameongezea kwa kusema, “tunakabiliwa na matarajio ya sutafahamu yanayoongezeka zaidi huko Ghaza, ambapo hakuna mtu aliye salama na hakuna mahali popote salama pa kwenda.”

Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amekumbusha kuwa operesheni ya ufikishaji misaada ambayo tayari ni tete inaendelea kudhoofishwa na miripuko ya mabomu, ukosefu wa usalama na kunyimwa watu fursa ya kufikiwa na misaada.

Griffiths amehitimisha tarifa yake kwa kusema: “haitoshi kwa miezi sita ya vita kuwa wakati wa ukumbusho na maombolezo, ni lazima pia kuchochea azimio la pamoja kwamba kuwe na uwajibikaji kwa usaliti huu dhidi ya ubinadamu”.../


342/