Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

8 Aprili 2024

20:11:48
1450077

WFP yatahadharisha kuhusu kuzidi kuwa mbaya hali ya watoto Ukanda wa Gaza

Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ametahadharisha kuwa watoto katika Ukanda wa Gaza wanapoteza maisha kutokana na njaa.

Asilimia 95 ya wakazi wa Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula; huku watoto wakiwa na hali mbaya zaidi. Watoto wengi walio na umri wa chini ya miaka mitano wa eneo hilo wana tatizo la utapiamlo. Hii ni katika hali ambayo hadi sasa watoto kadhaa waliojeruhiwa katika vita ambao walilazwa hospitalini kwa ajili ya matibabu huko Gaza wameaga dunia kwa tatizo la utapiamlo. 

Watoto, akina mama wajawazito, wanaonyonyesha na watu wenye ulemavu wako katika hatari zaidi ya kukumbwa na utapiamlo unaosababishwa na kukosa chakula. Hii ni kwa sababu Israel ingali inazuia kuingizwa kiwango cha kutosha cha misaada ya chakula na maji ndani ya Gaza; na mbali na kufanya hivi, utawala wa Kizayuni unaendelea kushambulia kwa makusudi maduka yanayooka mikate na bidhaa za kilimo.  

Cindy Mcain Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) amesema kuwa watoto wengi katika Ukanda wa Gaza wanaaga dunia kwa njaa na wale ambao bado wapo hai wamekonda sana kwa kukosa lishe na miili yao haina virutubisho muhimu. 

342/