Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

8 Aprili 2024

20:13:33
1450080

Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran: Kuendelea serikali ya Netanyahu ni kuendeleza vita Ukanda wa Gaza

Kamanda Mkuu wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuendelea kuhudumu serikali ya Beanjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kunafungamana na kuendelea vita huko Ukanda wa Gaza.

Meja Jenerali Sayyid Abdulrahim Mousavi Kamanda Mkuu wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliashiria jana pambizoni mwa Mkutano wa Kisayansi wa Fikra za Ulinzi za askari jeshi Luteni Jenerali shahidi Ali Sayad Shirazi katika Chuo Kikuu cha Uongozi na Makao Makuu ya Jeshi kuhusu jinai zinazofanywa na Wazayuni katika Ukanda wa Gaza na hatua ya viongozi wa Marekani ya kukwamisha utekezaji usitishaji vita na kuongeza kuwa utawala wa Kizayuni umekwama kwenye kinamasi huko Gaza. 

Kamanda Mkuu wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Licha ya uungaji mkono na himaya ya pande zote ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni katika vita dhidi ya Gaza, lakini Wazayuni hao maghasibu hawajapata mafanikio yoyote katika vita hivyo. Meja Jenerali Mousavi ameendelea kubainisha kuwa, Wazayuni wanafanya kila linalowezekana ili kuathiri nguvu na uwezo wa Hamas na kwa njia hiyo waiangamize harakati hiyo hata hivyo kundi jasiri na imara la Hamas limeendelea kupambana na kusimama imara kwa nguvu zote na Wazayuni hata wameshindwa kutimiza ahadi waliyotoa ya kuwakomboa mateka wao. Utawala wa Kizayuni umefanya mauaji makubwa huko Ukanda wa Gaza na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya raia wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina tangu Oktoba 7 mwaka jana kwa kuungwa mkono kwa pande zote na nchi za Magharibi hasa Marekani. Utawala wa Kizayuni umetekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Gaza huku jamii ya kimataifa na taasisi za haki za binadamu zikisalia kimya mbele ya jinai hizo za Israel na hivyo kuutia kiburi utawala huo haramu cha kuendeleza mauaji dhidi ya wanawake na watoto wa Kipalestina. 

342/