Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

8 Aprili 2024

20:13:54
1450081

Leo ni siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia nchini Iran

Leo, Jumatatu tarehe 8 Aprili mwaka 2024, imepewa jina la "Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia" kwa kutambua juhudi kubwa za kujifakharisha za wanasayansi wa nyuklia wa Iran katika kukamilisha mzunguko wa nishati ya nyuklia.

Wanasayansi wa Kiirani katika siku kama ya leo mwaka 2006 walifanikiwa kuzalisha mzungumko kamili wa fueli ya nyuklia katika kiwango cha maabara.  

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa nchi zinazomiliki teknolojia ya kurutubisha madini ya urani katika kalibu ya miradi yake ya nyuklia yenye malengo ya amani sambamba na kutangaza Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) habari ya mafanikio ya wanasayansi na wasomi wa Kiirani katika uwanja wa kumiliki teknolojia ya kurutubisha urani na kuanzisha mfumo kamili wa urutubishaji kupitia sentrifyuji zilizoundwa hapa hapa nchini Iran.   

Leo hii Iran inajivunia kuwa na kiwango cha juu zaidi cha ukuaji katika uzalishaji wa sayansi, na ni miongoni mwa nchi zenye elimu ya kisasa katika nyanja kama vile uzalishaji na uuundaji wa seli shina, nano teknolojia, na katika utengenezaji wa aina mbalimbali za dawa za matibabu kwa kutumia sayansi ya nyuklia.  

Muhammad Eslami Makamu wa Rais na Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ametuma ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia na kusema: Siku hii ni kama jani la dhahabu linalotokana na juhudi za usiku na mchana na endelevu za wanasayansi na wasomi watajika kwa ajili ya ustawi wa sayansi na teknolojia katika sekta ya nyuklia ya nchi hii.  

342/