Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

8 Aprili 2024

20:16:09
1450085

Iran: Tunaunga mkono mwenendo wa mazungumzo ya amani huko Yemen

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono mwenedo wa mazungumzo ya amani huko Yemen.

 Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekutana na kuzungumza huko Muscat mji mkuu wa Oman na Muhammad Abdulsalam mjumbe wa ngazi ya juu wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ambapo ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono mwenendo wa mazungumzo ya amani Yemen. Abdollahian amesema kuwa mashamulizi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen yanakiuka mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya nchi hiyo. 

 Amir Abdollahian amepongeza mshikamano wa Serikali ya Ukovu wa Kitaifa ya Yemen na Iran kuhusu shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Syria na kuongeza kuwa: Hakuna shaka kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na hatua za kisheria na kimataifa zinazochukuliwa, itatumia haki zake zinazotambulika ndani ya fremu ya sheria za kimataifa kuwajibu na kuwaadhibu wavamizi na watenda jinai hao. Kwa pande wake, Muhammad Abdulsalam amesema amefurahishwa na mazungumzo aliyofanya na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na kuongeza kuwa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa na watu wa Yemen wako pamoja kikamilifu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu jinai ya karibuni ya utawala wa Kizayuni ya kuwauwa shahidi washauri wa kijeshi wa Iran huko Damascus, Syria. 

 Mjumbe huyo wa ngazi ya juu wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amemepongeza pia uungaji mkono maalumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa taifa la Palestina na mhimili wa Muqawama na akasema, msimamo huo wa kijasiri ndio sababu inayozifanya Marekani, utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wao kuiwekea mashinikizo na kuishambulia Iran.    

342/