Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Aprili 2024

15:51:10
1450458

Guterres: 'Nimevunjika moyo' Waislamu huko Gaza hawawezi kusherehekea Idil Fitr

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema moyo wake "umevunjika" kuona Waislamu katika Ukanda wa Gaza unaokumbwa na vita na kwengineko pengine hawawezi kusherehekea ipasavyo siikukuuu ya Idil Fitr, baada ya kumalizika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika ujumbe wake wa video uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X leo Jumatano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea masikitiko yake kuhusu ukatili unaowaathiri Waislamu katika eneo lililozingirwa la Gaza huko Palestina, Sudan na kwingineko duniani.

"Kila mwaka, ninaitakia heri ya Idil Fitr jamii ya Waislamu duniani kote. Moyo wangu umevunjika nikijua kwamba huko Gaza, Sudan na maeneo mengine mengi -- kwa sababu ya migogoro na njaa -- Waislamu wengi hawataweza kusherehekea ipasavyo," Guterres amesema katika salamu zake za IdulFitr.Israel ilianzisha mashambulizi ya kikatili kwenye Ukanda wa Gaza, yakilenga hospitali, makazi ya raia na nyumba za ibada, baada ya harakati za Muqawama wa Palestina kufanya Operesheni ya Kimbunga ya al-Aqsa dhidi ya utawala huo ghasibu tarehe 7 Oktoba. Hadi sasa utawala huo haramu umeuwa zaidi ya Wapalestina 33,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Israel pia imezuia maji, chakula na kukata umeme kwa eneo la Gaza, na kulitumbukiza katika mgogoro mkubwa wa binadamu. Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema katika taarifa yake iliyotolewa leo Jumatano kwamba linakaribisha sikukuu hii ya idi kwa "mioyo iliyojaa huzuni" kutokana na vita vya Israel vya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu katika Ukanda wa Gaza.

342/