Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Aprili 2024

15:51:35
1450459

CNN: Kauli za Netanyahu kuhusu shambulio dhidi ya Rafah ni sauti za debe tupu

Televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza katika ripoti yake kwamba, matamshi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu uhakika wa shambulio dhidi ya mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza ni sautii za debe tupu na cha mchezo wa kuigiza.

CNN iliwanukuu maafisa waandamizi wa serikali ya Rais wa Marekani, Joe Biden, na kuripoti kuwa: Kauli za Netanyahu kuhusu shambulio dhidi ya Rafah ni mchezo wa kimaonyesho ili kuzuia kupinduliwa na kuondolewa madarakani baraza lake lake la mawaziri.

Kabla ya hapo gazeti la Politico liliandika katika ripoti yake likiwanukuu maafisa wa serikali ya Marekani na Wazayuni kwamba vitisho vya Netanyahu vya kushambulia Rafah vinachochewa na malengo ya kisiasa.

Ripoti ya Politico inasema, ikiwa kweli Waziri Mkuu wa Israel amepanga tarehe ya kuanza mashambulizi dhidi ya Rafah, ushahidi uliopo unaonyesha kuwa, bado hajatangaza tarehe hiyo kwa makamanda wa Ijeshi na maafisa wengine ambao wanapaswa kujua ni lini operesheni hiyo itaanza na jinsi itakavyofanyika.

Madai ya kupangwa tarehe ya shambulio la Israel huko Rafah yanatolewa na Waziri Mkuu wa utawala huo wa Kizayuni, huku Rais Joe Biden wa Marekani akikiri Jumanne jioni kwamba sera za Israel huko Gaza zimefeli na kushindwa.

342/