Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Aprili 2024

15:52:12
1450460

UN yalaani Israel kwa kuwazuia waandishi wa habari kufika Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameikosoa Israel kwa kuwanyima waandishi wa habari wa kimataifa idhini ya kuingia katika Ukanda wa Gaza unaokumbwa na vita na kusema hatua hiyo inalenga kuficha ukweli.

Antonio Guterres siku ya Jumanne alitaja kuzuiliwa kwa waandishi wa habari kuingia Gaza kuwa ni hatua inayowezesha kuenea "taarifa potofu na simulizi za uwongo kushamiri."

Guterres alisema katika chapisho kwenye X kwamba kuwanyima waandishi wa habari wa kimataifa idhini ya kuingia Gaza ni kuruhusu habari potofu na hadithi za uwongo kustawi,"

Ameyasema hayo siku moja baada ya Jumuiya ya Wanahabari wa Kigeni, shirika linalowakilisha waandishi wa habari wanaofanya kazi huko Gaza, kuripoti kuwa Israel inaendelea kuwazuia waandishi wa kimataifa kuingia katika eneo hilo lenye vita."Israel inaendelea kuwazuia waandishi wa habari wa kimataifa kuingia katika sehemu yoyote ya Ukanda wa Gaza kwa uhuru," taarifa iliyotolewa na FPA ilisema siku ya Jumatatu, na kuongeza kuwa uamuzi huo unaibua maswali kuhusu masuala ambayo Israel inataka kuwaficha waandishi wa habari wa kimataifa. Upinzani wa jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza katika vyombo vya habari vya dunia na wimbi la upinzani na lawama za kimataifa kuhusu jinai hizo zimeufanya utawala wa Kizayuni kufunga mara moja kituo cha Televisheni ya Al-Jazeera katika Ukanda wa Gaza kutokana na jinsi kinavyoakisi habari za mauaji ya kimbari ya utawala huo katika vita hivyo. Israel inayodaiwa kuwa nembo ya demokrasia katika Mashariki ya Kati, inakiuka waziwazi uhuru wa kusema na wa vyombo vya habari kwa kuwaua waandishi wa habari na kufunga televisheni huru katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

342/