Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Aprili 2024

15:52:40
1450461

Wanamuqawama wa Iraq washambulia maeneo 5 ya utawala wa Kizayuni

Ripoti kutoka Iraq zinasema kuwa wapiganaji wa Muqawama wa Kiislamu wa Iraq wameshambulia maeneo matano ya Israel katika kuwaunga mkono raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza, ambao wanakabiliwa na vita vya kikatili na mauaji ya kimbari ya utawala ghasibu wa Kizayuni.

Muqawama wa Iraq umetangaza kuyapiga maeneo matano ya utawala haramu wa Israel katika taarifa yake ya leo asubuhi. Taarifa hiyo imeeleza kuwa Muqawama wa Iraq umefanya mashambulizi dhidi ya maeneo 5 ya Israel katika hatua mtawalia za kupinga ukandamizaji na uvamizi wa Israel dhidi ya raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza wakiwemo watoto, wanawake na wazee. Wapiganaji hao wa Iraq, waliojiunga na kundi mwavuli la Muqawama wa Kiislamu nchini humo linalopambana dhidi ya ugaidi, wameyapiga maeneo matano ya Israel katika kuonyesha mshikamano wao kwa wananchi wa Palestina wa Ukanda wa Gaza. Kundi hilo limesema, limetuma "silaha zinazofaa" dhidi ya shabaha ambazo ni pamoja na "bandari ya mafuta ya Ashkelon" katika sehemu ya kati ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kituo cha anga cha Hatzerim katika mji wa Beersheba kusini kati mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha vita dhidi ya watu wa Gaza Oktoba 7 mwaka jana kufuatia oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa iliyotekelezwa na makundi ya Muqawama ya Palestina dhidi ya maeneo kadhaa ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Wapalestina zaidi ya 33,200 wameuliwa shahidi katika mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel; aghalabu yao wakiwa ni wanawake na watoto.

342/